Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akijaribu moja ya
vidani vilivyotokana na kazi za wajasiriamali wasanii alipotembelea banda la
Mjasiriamali wakati wa kufunga tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akihutubia wageni
mbalimbali waliohudhuria kilele cha Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
....................................
NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza
amesema Serikali itaendelea kuwajengea uwezo, umahiri na ubunifu wasanii
wa Tanzania kupitia Mradi wa Utambuzi wa Wasanii wa Sanaa za Ufundi (TASIP) ili
kukuza soko la tasnia hiyo katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.
Akifunga Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, Wilayani Bagamoyo,
Mkoani Pwani jana (Jumamosi Oktoba 27, 2018), Shonza alisema malengo ya
Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa tasnia ya sanaa nchini inapiga
hatua kubwa zaidi na kuwafanya wasanii kunufaika na kazi zao.
Aliongeza kwa kuzingatia kuwa Wizara yake inasimamia na kutekeleza
sera ya sanaa nchini, Serikali itahakikisha kuwa kuipitia mradi wa TASIP
unawafikia na kuwatambua wasanii wote nchini na kuwawezesha kuwa na utambulisho
rasmi utawaozesha kupata mitaji na mikopo ya kuendesha shughuli zao.
“Mwaka jana nilizindua mradi huu wa TASIP na mwaka huu tumeanza kushuhudia
mafanikio makubwa kupitia program hii, kwa kuwa wapo baadhi ya wasanii
waliotambuliwa na kusajiliwa na wameanza kupata mikopo kutoka mabenki hatua
inayowezesha kupata kutatua baadhi ya changamoto katika kuendesha shughuli zao”
alisema Shonza.
Naibu Waziri Shonza alisema Serikali itaendelea kutoa msukumo kwa
wafadhili mbalimbali kuweza kuunga mkono Tamasha la Sanaa na Utamduni Bagamoyo
linalofanyika kila mwaka nchini, kwa kuwa Tamasha hilo linawezesha wasanii wa
Tanzania wanapata uzoefu wa masuala mbalimbali kutoka kwa wasanii wenzao wa
mataifa mbalimbali ya nje na hivyo kuweza kuongeza ubunifu katika kazi zao.
Kwa mujibu wa Shonza alisema kwa kutambua umuhimu wa Tamasha hilo,
Serikali itaendelea kuijengea Tasasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA)
kwa ili kuwa na uwezo kuweza kuzalisha wasanii na wakufunzi wenye ubora
katika ngazi ya kitaifa na kimataifa kwani Taasisi hiyo imekuwa kiungo muhimu
cha uzalishaji wa wasanii katika mataifa mbalimbali ya kigeni.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akisaini kitabu
cha wageni mara baada ya kutembelea Banda la Bodi ya Filamu na Michezo ya
Kuigiza Nchini wakati wa kilele cha Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. Kulia
kwakeni Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo, Joyce Fisoo na Kushoto ni Mwenyekiti wa
Bodi hiyo, Prof. Frowin Paul Nyoni.
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fisoo, Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi
hiyo Prof. Frowin Paul Nyoni na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Bodi ya
Utalii Tanzania (TTB) Geofrey Tengeneza, wakibadilishana mawazo wakati wa
kufungwa kwa Tamsha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba
27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fisoo akitoa ufafanuzi kuhusu
matumizi ya vitambulisho rasmi vya Bodi hiyo kwa watayarishaji na waandajii wa
filamu mbalimbali nchini kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Juliana Shonza wakati alipotembelea banda la Bodi hiyo katika kilele
cha Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Oktoba 27, 2018, Wilayani
Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (katikati)
akipata maelezo kutoka kwa Mjasiriamali wa sanaa za uchongaji, Ras Jeshi
Beku alipotembelea banda la Msanii huyo wakati wa kufunga tamasha la 37
la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani
Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
No comments:
Post a Comment