Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akikagua stendi mpya ya mabasi Kibaha .
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.
.....................................
NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA
MAKAMU wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekataa kuzindua
stendi kuu mpya ya Mailmoja Kibaha mkoani Pwani, akiwa katika ziara yake mkoani
humo.
Hatua hiyo ameifikia kutokana na kupata wasiwasi wa utekelezaji wa mradi
kuwa na baadhi ya mapungufu ambapo amedai baada ya kufanya uchunguzi wiki mbili
ama tatu zijazo atakwenda kuuzindua.
Akizungumza katika stand hiyo, Samia alieleza, kuna minong’ono wameisikia
kuhusu mradi huo hivyo ni jukumu lake kuibeba na atakapo jiridhisha atarudi kwa
mara nyingine .
Hata hivyo, alisema atakutana na mkuu wa wilaya, mkurugenzi na mkuu wa
mkoa kuzungumzia suala hilo.
“Msishtuke kwa hili ni kawaida kwa kuchukua hatua za aina hii ili
kujiridhisha kwa maslahi ya halmashauri, mkoa na watumiaji kijumla “
“Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni sikivu na kusikia malalamiko ya
wananchi, tumepata malalamiko kidogo kuhusu stand hii, serikali ni ya uwazi na
ukweli hivyo sitofungua stendi “alisisitiza Samia.
Samia alimpongeza mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kibaha, Jennifer
Omolo na mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama na wahusika waliohusika
kufanikisha mradi huo.
Nae waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa
-TAMISEMI ,Selemani Jafo alisema yeye kama waziri wapo wataalamu wanaohakiki
lakini ameridhishwa na kazi hiyo .
“Kwani kila kazi ina changamoto za kibinadamu, hasi na chanya,
lakini wamejitahidi “alisema Jafo.
Jafo alieleza, mradi huo umepata msaada wa mkopo nafuu kutoka bank ya
Dunia ambao wamepata fedha za kimarekani dollar milioni 255 .#
Alielezea , wanagusa miji 18 na wanachokifanya wanagusa stendi tisa,
barabara za miji kwa kiwango cha lami na madaraja makubwa ya kisasa.
Wakitoa kero ya stand hiyo, madereva pikipiki walidai eneo lililotengwa
kwa ajili yao halina sehemu ya kujikinga hivyo kusababisha usumbufu wakati wa
mvua na jua.
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kibaha, Jennifer Omolo alisema katika
stendi ndogo ya awali walikuwa wakikusanya ushuru sh. 950.000 kwa siku
ambapo sasa wanakusanya sh. milioni 1.6 .
Alisema mradi huo umegharimu sh. bilioni 2.9 na walishamlipa mkandarasi
bilioni 2.7 ,stendi hiyo itakuwa na mabanda kumi ya kukatia tiketi, mawakala 40
,eneo la tax, na wafanyabiashara ndogondogo wanaojiingizia kipato kwa kuuza
biashara zao wapo 100 .
Samia akiwa katika ziara yake Kibaha vijijini na mjini pia alipata fursa
ya kutembelea mradi wa reli ya kisasa ya standard gauge kujionea namna
unavyoendelea.
No comments:
Post a Comment