Kaimu
Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Hassan Musa Kabeke akizungumza na wajumbe wa
halmashauri ya BAKWATA mkoani Mwanza, masheikhe wa wilaya, Kata na Misikiti ya
wilaya zote za Mwanza jana, kwenye ukumbi wa mikutano wa baraza hilo Mbugani
katika Wilaya ya Nyamagana jana. Picha na Baltazar Mashaka.
....................................
NA
BALTAZAR MASHAKA, MWANZA.
KAIMU
Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza Hassan Musa Kabeke amesema moja ya vipaumbele vyake
ni kuimarisha uchumi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na elimu ya
dini.
Sheikhe
Kabeke alitoa kauli hiyo jana kwenye ukumbi wa ofisi za BAKWATA zilizopo
Mbugani katika Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, wakati akizungumza na wajumbe
wa halmashauri ya mkoa, masheikh wa wilaya na kata mkoani humu.
Alisema
miongoni mwa mambo yanayomkera ni hali duni ya maisha na udhalili (unyonge)
hivyo ameweka mikakati na mipango ya kuimarisha uchumi wa BAKWATA ili
kubadilisha maisha ya walimu wa madrasa, masheikhe na maimamu wa misikiti ambao
ni zao la uislamu (kiwanda) na misingi ya dini hiyo ya Kiislamu.
Kaimu
Sheikhe huyo wa mkoa alisema madrasa na msikiti ndio eneo dhaifu kutokana na
walimu na masheikhe kushindwa kufundisha elimu ya dini na hata ujira wao ni
mdogo wanazidiwa na watumishi wa ndani jambo ambalo linamkera na hivyo ameamua
kulitafutia tiba.
Sheikhe
Kabeke alieleza kuwa ili kuboresha hali za walimu wa madrasa,masheikhe na maimu
na waumini wa kiislamu lazima kuwe na vyanzo vya mapato yatakayosaidia Waislamu
na haiwezekani kuendelea kuwa na BAKWATA ombaomba.
“Niwaondoe
hofu maana wapo watu wanaosema mimi ni mkali la hasha, mimi nina msimamo kwenye
haki.Sote tunachukia ufisadi, wizi na umaskini na hata Mufti wa Tanzania kilio
chake ni kutaka kuwatoa waislamu kwenye udhalili (unyonge).Katika hili la
kuimarisha uchumi hata mkinilaumu niko radhi na Mwenyezi Mungu
atanihukumu,”alisema Sheikhe Kabeke.
Alisema
waislamu hawana sababu ya kuwa wanyonge na wasimuone mkali bali atautumia na
kuendelea na ukali huo kuwaondoa kwenye unyonge wao kuwataka viongozi dini ya
kiislamu na waumini kutumia neema waliyopewa na Mungu kutafuta pepo na
nyumba ya ahera.
Aliongeza
kuwa BAKWATA ina hali mbaya kiuchumi na ni taasisi pekee isiyo na wanachama
wanaolipa ada wakati chombo hicho kinawapa heshima hivyo kwa Mkoa wa Mwanza
dira na mipango yake ya kuleta maendeleo viongozi wa ngazi ya mkoa watachangia
sh.8,000 mwezi sawa na sh. 2,000 kwa wiki fedha ambazo zitawekwa kwenye akaunti
maalumu.
“Tunataka
kujenga uchumi kwa kuangalia rasilimali watu na kuanzia Oktoba viongozi
watachanga sh. 8,000 kwa ngazi ya mkoa, wilaya sh. 4,000 , kata sh.
500 na tayari akaunti imefunguliwa kwa usalama wa fedha hizo ili ndani ya miaka
tujenge jengo la kitega uchumi, kulipa mishahara ya walimu wa madrasa na
masheikhe na kutatua kero zao,” alifafanua Sheikhe Kabeke.
Aidha,kuhusu
elimu ambayo imegawanyika sehemu tatu, aliwawataka waislamu kuacha kulalamika
kuwa taasisi yao inahujumiwa na kuchafuliwa pamoja na kupoteza akidi yao ilhali
wenye dhamana ya kufundisha elimu ya dini shuleni hawatimizi wajibu wao
na kusababisha vijana waliolelewa kwa misingi ya dini kiislamu wakosekane.
Alisistiza
kuwa kama huo ni ukali basi hana budi kuacha hali iendelee ili uislamu ufe na
kutoweka kwa sababu masheikhe na walimu hawaoni umuhimu wa kufundisha elimu ya
dini shuleni licha ya kutengwa kwa vipindi vya dini.
Kaimu
Sheikh huyo wa mkoa alimshukuru Mufti wa Tanzania Abubakar Zuberi bin Ali
kwa na Baraza la Ulamaa kwa kumteua, kumuona na kumuamini kuwa anafaa kumsaidia
kwenye nafasi hiyo kubwa ambayo si ya kukimbiliwa na kuahidi kuwa kwenye
uongozi wake hatabadilika na atakubali kushauriwa.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya BAKWATA Mkoa wa Mwanza Amran Batenga akizungumza na wajumbe
wa halmashauri hiyo, masheikhe wa wilaya na kata za mkoani humu jana kwenye
ukumbi wa baraza hilo Mbugani katika Wilaya ya Nyamagana.
Kaimu
Katibu Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza, sina Mwagalazi
akizungumza na wajumbe wa Halmashauri kuu ya baraza hilo, masheikhe wa wilaya
na kata wa wilaya za mkoani humu.
No comments:
Post a Comment