Mkuu
wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akizungumza na wananchi (hawapo Pichani) wa
Tarafa ya Nguruka wilayani Uvinza mkoani Kigoma Jana 24/10/2018, na kuwataka
kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kufichua uhalifu na wahalifu
pamoja na watu wanaojihusisha na matukio ya mauaji ili waweze kuchukuliwa hatua
kali za kisheria.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Uvinza
Mhe. Mwanamvua Mlindoko, wakati alipowasilia wilayani Uvinza Tarafa ya Nguruka
mkoani Kigoma Jana 24/10/2018, kwa lengo la kuzungumza na wananchi kufuatia
tukio la kushambuliwa na kuuawa kwa askari wawili na wingine mmoja kujeruhiwa
wakati wakitekeleza zoezi la kuwaondoa wananchi waliovamia eneo la Ufugaji
Ranchi ya Taifa NARCO kwa kuendesha shughuli za kilimo kinyume cha sheria na
taratibu za nchi.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akiondoka baada ya kumaliza mkutano na
wananchi wa Tarafa ya Nguruka wilayani Uvinza mkoani Kigoma Jana 24/10/2018,
ambapo IGP Sirro, aliwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa sahihi
zitakazofanikisha kukamatwa kwa watu waliojihusisha na tukio la kuwashambulia
na kuwaua askari wawili na wananchi wawili wilayani humo. PICHA NA JESHI LA POLISI.
No comments:
Post a Comment