Inspekta
Jenerali wa Polisi Tanzania IGP Saimon Sirro akionyesha mbele ya waandishi wa
habari moja ya silaha mbili aina ya Bastola
ziliyopatikana kwenye gari lililohusika katika utekaji wa mfanyabiashara
Mohamed Dewji Oktoba 11 mwaka huu katika hoteli ya Collesium jijini Dar es
salaam.
..............................
KAMANDA wa Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema kuwa baada ya kupatika
kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji Moo. Jeshi la polisi linaendelea na msako
kuhakikisha waliokuwa wamemteka mfanyabiashara huyo wanapatikana popote walipo.
Kamanda Sirro amesema kuwa atahakikisha watekaji hao wanapatikana wakiwa
hai au wamekufa huku akitoa onyo kali kwa vikundi ambavyo vinaingilia majukumu
ya jeshi hilo nakubainisha kwamba anamashaka na uraia wao.
IGP Sirro ameyasema haya wakati akizungumza na waandishi wa habari Makao
makuu ya Jeshi la Polisi ambapo amesema katika kuhakikisha wanapoteza
ushahidi walijaribu kuliunguza Gari hilo ambalo lilikuwa limetelekezwa katika
eneo la Ghymkana.
Amesema taarifa za kupatikana kwa Mohamed Dewji zilitolewa na
Askari wa Getini katika eneo hilo la Ghymkana ambapo Mo alimtaka
Askari huyo kutoa taarifa kwa familia yake ndipo walipokuja katika eneo
hilo.
Amesema kuwa baada ya kuja katika eneo hilo ndipo walipojulishwa Polisi
nawenyewe kufika katika eneo la tukio na kujiridhisha kupatikana kwa
Mfanyabiashara huyo Dewji.
“Ilikuwa majira ya saa saba usiku Maeneo ya Gymkhna gari aina ya Toyota
Sulf Lilitelekezwa ndani yake likiwa na mfanyabiashara Mohamed Dewji
ambapo baada ya kumwacha katika eneo hili walijaribu kutaka kupoteza ushahidi
kwa kulichoma moto gari ambalo lilimbeba.” amesema Sirro.
Akifafanua zaidi amesema Gari hilo ni lile ambalo alilionyesha mbele ya
waandishi wa habari mapema wiki hii. gari lenye namba za usajiri T314AXX
Na kwenye vioo vya pembeni kulikuwa na namba za usajili AGX 404 MC yenye rangi
ya blue nyeusi na ufito wa rangi ya shaba kwa chini.
Kamanda Sirro amesema kuwa baada ya kufanya mazungumzo na Mo Dewji
aliwaeleza waliomteka walikuwa wanazungumza lugha ya kingereza na mmoja lugha
ya kiswahili cha hovyo.
Kwamujibu wa kamanda sirro amesema Mo aliwaeleza kuwa baada ya kumteka
walitaka atoe fedha ambapo aliwaeleza yeye alikuwa hana hela na badala yake
aliwaeleza awape namba za simu za baba yake.
Amesema hata walipopewa na za simu za baba yake hawakuweza kumpigia bila
shaka waliogopa mtego wa polisi hivyo.” Sisi kama polisi tunashukuru Mo
kapatikana lakini Jeshi la Polisi tutaendelea na msako na tunawataka
wananchi.kuendelea kushirikiana nasi ili kuhakikisha tunakomesha matukio
haya.”amesema Sirro.
Pia Kamanda Sirro amesema kuwa atahakikisha waliomteka Mo Dewji
wanakamatwa .tena wakiwa hai au wamekufa ili kukomesha vitendo hivi na taifa
kuendelea kuwa mahala salama wakati wote.
Katika hatua nyingine Kamanda Sirro ametoa Onyo kali kwa kikundi cha
baadhi ya watu ambao wanaingilia utendaji wa Jeshi la Polisi kupitia mitandao
ya kijamii.
” Kuna kikundi ambacho chenyewe kipo kwa ajili ya kuingili majukumu ya
polisi jamani Polisi wanafanya kazi usiku kucha tena wakipita kukagua katika
kila eneo nakwamba wenyewe wamelala na wake zao lakini kazi yao kuingilia kazi
za polisi.”amesema Sirro.
Pia amezitaja baadhi ya nchi ambazo wanashirikiana kuhakikisha watekaji
wanatiwa nguvuni.ambazo ni Afrika kusini,kenya,Uganda,Msumbini,…nakwamba ndani
ya siku tisa askari wake hawajalala kuhakikisha Mo anapatikana.
Mo Dewji alitekwa Oktoba 11,2018 majira ya alfajiri katika Hoteli ya
Colessum iliyopo masaki ambapo mara zote amekuw akifanya mazoezi ya Gym.
Hizi
ndiyo silaha AK 47 moja na bastola tatu zilizopatikana kwenye gari lililohusika
katika tukio la utekaji wa mfanyabiashara Mohamed Dewji hivi karibuni jijini
Dar es salaam.
Gari
lililohusika katika utekaji huo lililokutwa eneo la Gymkana jijini Dar es
salaam.
No comments:
Post a Comment