Sunday, October 28, 2018

PANGANI WAJIWEKA TAYARI KWA ZIARA YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

MWENYEKITI wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Seif Ally akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Pangani
.................................


MKUU wa wilaya ya Pangani mkoani Tanga Zainabu Abdallah amewataka viongozi na wananchi wa wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye mapokezi ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anayetarajiwa kuanza ziara wilayani humo Octoba 29 mwaka huu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari Mkuu wa wilaya hiyo mara baada ya kumalizika kikao cha maandalizi ya ziara hiyo aliwataka wananchi hao wakiwemo viongozi kujitokeza kwa wingi eneo la Mkwaja kwenye mapokezi hayo.

Alisema baada ya mapokezi hayo Waziri Mkuu anatarajiwa kuzungumza na wananchi kwenye maeneo ya Sakura,Mwera na Bomani Pangani mjini huku wananchi wakitakiwa kujumuika kwenye mikutano hiyo kwa wingi.


Hata hivyo aliwataka wananchio  kutumia fursa hiyo kwenda kumsikiliza Waziri Mkuu na kuwasihi wale watakaopata nafasi endapo itatolewa kuitumia kusema kwa niaba ya wana Pangani wengi na kueleza changamoto zao na kuzungumza na kiongozi wao aliekuja kwa ajili yao.


Katika hatua nyengine Mkuu wa Wilaya ya Pangani Zainab Abdallah kwenye muendelezo wa tamaduni ya ushirikiano na mshikamano wa viongozi katika wilaya ya Pangani amekutanisha  pamoja viongozi wote kwa kushirikisha Kamati ya ulinzi na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya,Halmashauri ya Wilaya ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Seif Ally,Mkurugenzi na wakuu wote wa Idara,Taasisi zote,Ofisi ya Mbunge,Kamati ya siasa ya chama Tawala(CCM),Madiwani wote,NGO’s,Viongozi wa Dini na viongozi wengine wote.

Lengo ni kuunganisha nguvu ya pamoja na kujiweka tayari kupokea ugeni mkubwa na wa heshima unaotarajiwa kutua wilayani hapa October 29 mwaka huu siku ya Jumatatu.

 

Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Hassani Nyange akizungumza katika kikao hicho

Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George akizungumza katika kikao hicho

No comments:

Post a Comment