Mbunge wa jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa, akikabidhi Jezi kwa moja ya timu zilizowahi kushiriki mashindano ya Kawambwa Cup katika jimbo hilo.
.....................................................
Na
Omary Mngindo, Kitame- Oktoba 23
TIMU
ya soka ya Kitame Fc ya Kijiji cha Kitame, Kata ya Makurunge Jimbo la Bagamoyo
Mkoa wa Pwani imemtaka Mbunge wao Dkt. Shukuru Kawambwa kurejesha michuano ya soka
ya Kawambwa Cup.
Wakizungumza
kwenye mkutano ulioandaliwa na mbunge wao, nahodha wa timu hiyo Daniel Joseph
na Mwenyekiti Salehe Ismail wamesema kuwa kusimama kwa mashindani hayo
yamewakosesha vijana kuonesja uwezo wao, hivyo kudumaza vipaji.
Nae
Ismail alisema kuwa michuako hiyo iliyokuwa inachezeshwa kwa miaka kumi
mfululizo, yakishirikisha timu mbalimbali kwa kiasi kikubwa ilisaidia kuibua
vipaji vya vijana ambapo baadhibyao wanefanikiwa kucheza ligi mbalimbali.
"Mbunge
tunakuomba ufanye juu chini uturudishie mashindano ya Kawambwa Cup, katika
kipindi chote cha miaka kumi timu zetu zililuwa zinashiriki michuano hiyo
kuanzia ngazi za Vijiji, Kata hatimae hatua ya Kawambwa Cup," alisema
Mwenyekiti hiyo.
Akijibia
maombi hayo, Dkt. Kawambwa alisema kuwa yupo katika mikakati ya kuhakikisha
kuanzia mwanzoni kwa mwaka ujao wa 2019 yaanze kama ilivyokuwa hapo awali.
"Ni
kweli michuano ya Kawambwa Cup iliyochezwa kwa miaka kumi mfululizo yalikuwa na
hamasa mkubwa, vijana walipata fursa ya kuonesha vipaji vyao, Niko mbioni kuona
no namna gani yaweze kuchezwa kuanzia mwakani," alisema Kawambwa.
Alisema
kuwa kukosekana kwa michuano hiyo katika kipindi kifupi hata kwake
hakijamfurahisha na lwba imetokana na kutokuwa katika mazingira mazuri ya
kifedha.
No comments:
Post a Comment