Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Ripoti ya Kamati iliyoundwa na Serikali
Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere kutoka kwa Mwenyekiti wa
Kamati hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstafu, Jenerali George
Waitara, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Ripoti ya Kamati iiyoundwa na
Serikali Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere baada ya
kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu,
Jenerali George Waitara (kushoto) kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es
salaam, Oktoba 25, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati iliyoundwa na
Serikali Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere baada ya kupokea Ripoti
ya Kamati hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 25,
2018. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera na Uratibu, Profesa
Faustin Kamuzora na wapili kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali George Waitara.(Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
...............................
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea ripoti ya uchunguzi
wa ajali ya kivuko cha MV Nyerere kutoka kwa kamati iliyoundwa na
Serikali kwa ajili ya kuchunguza ajali hiyo.
Amepokea ripoti hiyo leo (Alhamisi, Oktoba 25, 2018) kutoka kwa
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstafu,
Jenerali George Waitara,kwenye makazi ya Waziri Mkuu, jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuishikuru kamati hiyo kwa niaba ya Rais
Dkt. John Magufuli kwa kazi kubwa waliyoifanya ambayo imethibitisha umakini
wao.
Pia ameipongeza kamati hiyo kwa namna walivyotumia muda wao vizuri kwa
kufanya kazi hiyo na kutoa mapendekezo kwa Serikali juu ya mambo waliyoyabaini.
“Nimepokea taarifa kwa niaba ya Serikali, Serikali itafanya mapitio ya
taarifa yote na viambatisho vyake na itapitia kwa kina mapendekezo mliyoyatoa
ambayo yote yatafanyiwa kazi.”
Waziri Mkuu ameongeza kuwa Serikali inaamini mambo yote yaliyosheheni
katika taarifa hiyo ni yale ambayo Watanzania wanasubiri kuona yakifanyiwa
kazi.
MV Nyerere ilipindika na kuzama Septemba 20, mwaka huu katika ziwa
Victoria ambapo Watanzania zaidi 200 walipoteza maisha na wengine Zaidi ya 40
waliokolewa.
Septemba 24 mwaka huu Waziri Mkuu alitangaza kamati ya kuchunguza ajali
ya kivuko cha MV Nyerere yenye wajumbe saba ambayo iliyoongozwa na Jenerali
mstaafu, Waitara.
Akitangaza majina hayo kwenye kijiji cha Bwisya katika kisiwa cha Ukara,
wilayani Ukerewe, mkoani Mwanza, Waziri Mkuu alisema wajumbe hao
wanapaswa kuikamilisha kazi hiyo ndani ya mwezi mmoja.
Aliwataja wajumbe wengine ni aliyekuwa Mbunge wa Ukerewe, Bw. Joseph
Mkundi, Mhandisi Marcelina Magesa, Wakili Julius Kalolo na Katibu Mkuu wa Umoja
wa Wanawake Tanzania (UWT), Bi. Queen Mlozi.
Wengine ni SACP Camillus Wambura na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Uratibu Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Bashiru Taratibu Hussein.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa
Kamati iliyoundwa na Serikali Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha MV
Nyerere baada ya kupokea Ripoti ya Kamati hiyo kwenye Makazi ya
Waziri Mkuu, jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018. Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Katibu
Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustin
Kamuzora na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi
Mstaafu, Jenerali George Waitara. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mwenyekiti wa
Kamati iliyoundwa na Serikali Kuchunguza Ajali ya Kivuko
cha Mv Nyerere, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali, George
Waitara baada ya kupokea Ripoti ya Kamati hiyo kwenye Makazi ya
Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
No comments:
Post a Comment