Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata
maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja
(kulia) ya miundo mbinu ya maji itakavyokuwa mara baada ya kukamilika kwa
ujenzi wa tanki la maji litakalokuwa na uwezo wa kubeba lita milioni 6, Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo kwenye ziara ya kuhamasisha
shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani.
..................................
..................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan amesema Serikali ya awamu ya tano imeendelea kutekeleza ahadi ya
kusambaza maji mjini na vijijini ambapo mpaka ifikapo mwaka 2020 inategemea
maji yatakuwa yamefika vijijini kwa asilimia 85% na mjini asilimia 90%.
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa
tanki kubwa la mradi wa maji Bagamoyo lenye uwezo wa kubeba lita milioni 6
ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya siku sita mkoani Pwani.
Makamu wa Rais ameipongeza Dawasa kwa kazi nzuri na amewataka wananchi
kupitia kamati mbali mbali za maji kutunza na kuvilinda vyanzo vya maji, miundo
mbinu pamoja na mazingira yake.
“Wote tujitahidi kutunza vyanzo vya maji” alisema Makamu wa Rais
Tenki hilo la Bagamoyo linatarajiwa kuhudumia wakazi wote wa mji wa
Bagamoyo na vitongoji vyote vinavyozunguka mji huo.
Makamu wa Rais pia alipata nafasi ya kutembelea mradi wa uzalishaji na
usambazaji vifaranga wa kampuni ya AKM Glitters na kuzungumza na wananchi waliojitokeza
kwenye viwanja vya shule ya msingi Majengo.
Katika ziara hiyo Makamu wa Rais aliongozana na Naibu Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu na
vIongozi wengine wa Chama na Serikali.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) ya miundo mbinu ya maji itakavyokuwa mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa tanki la maji litakalokuwa na uwezo wa kubeba lita milioni 6, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza
na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) na Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati wa kukagua Mradi tanki la
maji Bagamoyo litakalokuwa na uwezo wa kubeba lita milioni 6, Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za
kimaendeleo mkoani Pwani.
No comments:
Post a Comment