Saturday, October 20, 2018

RC SHINYANGA AKAGUA MRADI WA UPANUZI KITUO CHA AFYA.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akikagua ubora wa matofali yalitengendezwa kwa ajili ya kujenga majejngo ya kituo cha afya Kishapu kinachofanyiwa upanuzi.
..........................

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack amekagua mradi wa upanuzi wa kituo cha afya Kishapu ulioanza kutekelezwa katika Wilaya ya Kishapu.

Akiwa katika mradi huo kituoni hapo wenye thamani ya sh. milioni 400 Mhe. Telack alitaka nguvu za wananchi zishirikishwe katika ujenzi wa vituo vya afya.

Sanjari na hilo aliwataka wataalamu waziache kamati za ujenzi zifanye kazi ya kusimamia miradi hiyo ya ujenzi wa vituo vya afya.

“Wataalamu msiingilie hizo kamati na tunachotaka ni majengo imara, tofali imara, simenti iwe haijaexpire (haijakwisha muda wake), agizeni kwa bei ya jumla na nafuu itatusaidie kujenga kituo,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa alikutana na Kamati ya Lishe Wilaya ya Kishapu na kuwataka wataalamu hao kutoa elimu ya lishe kwa wananchi ili kuondoa udumavu.

Aliagiza fedha zinazotengwa kwenye bajeti kwa ajili ya masuala ya lishe zisimamiwe vizuri ili kuhakikisha zinafanya kazi hiyo lishe.

“Kila mtu kwa nafasi yake akifanya kile kinachotakiwa kufanyika mkoa wetu  utasimama vizuri ka hiyo kila mmoja kwa jukumu lake,” alisisitiza Mhe Telack.


No comments:

Post a Comment