MAKAMU wa Rais Mama Samia Hasan Suluhu akizungumza katika Halmashauri ya Chalinze wakati wa ziara yake wilayani Bagamoyo, Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete.
........................................................
Na Shushu Joel,Chalinze.
MAKAMU wa Rais Mama Samia Hasan Suluhu ameipongeza halmashauri ya wilaya
ya chalinze iliyoko wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kwa utekelezaji wake
wa miradi bora ya Afya yenye lengo la kumaliza changamoto za hupataji wa huduma
za kiafya kwa wakazi wa maeneo hayo.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Lugoba mara baada ya kutembelea kituo
cha afya cha lugoba kinachojengwa na serikali ya awamu ya tano,Mama Samia
alisema kuwa chalinze ni mfano wa kuigwa kutokana na kile ambacho serikali
imekuwa ikisisitiza kufanyika kwa wananchi wake basi chalinze kinafanyika kwa
mifano na huu ndiyo utekelezaji wa ilani tulioubiri mimi na Raisi Magufuli
wakati tunaomba kuungwa mkono.
“Nimejionea mwenyewe jinsi chalinze inavyotekeleza na kusimamia fedha za
serikali kwa makusudi yale iliyokuwa ikiyahitaji yafanyike kwa wananchi wake
inavyotekelezeka kwa vitendo kwenye halmashauri hiyo”Alisema Mama Samia Suluhu.
Aliongeza kuwa usimamizi unaofanywa na wasaidizi wa serikali kupitia
mwakilishi wa wananchi mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete umekuwa ni wa
tija katika kutambua thamani ya wananchi wao katika kuwafanikishia maendeleo.
Aidha Mama Samia Suluhu ametumia mkutano huo kuwataka wananchi wa
chalinze na hasa kinamama kujijengea tabia ya kuwahi mapema katika vituo vya
afya pindi wanapokuwa wajawazito ili kuweza kupata ushauri nasaha kutoka kwa
wataalamu na kuacha tabia za kutumia miti shamba ambayoinaweza sababisha
matatizo makubwa kwa wakina mama wakati wa kujifungua.
Pamoja na wito huo, Makamu wa Raisi aliwakumbusha Wananchi wa Halmashauri
ya Chalinze kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa, kwani faida ya Mfuko
huo ni kubwa sana. Mfuko wa Bima ya Afya utawawezesha wananchi kutibiwa hadi
Hospitali kubwa za Rufaa, Jiungeni na fursa hii ili kulinda na kuhifadhi afya
zetu.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete amempongeza Raisi
Dr.John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu kwa kutambua
jitihada zinazofanywa na viongozi wa chalinze katika ufanikishaji wa miradi ya
maendeleo hasa katika sekta ya afya,elimu,maendeleo ya jamii na maeneo mengine
ya ustwi wa jamii.
Mheshimwa Kikwete, Alisema kuwa mpaka sasa jimbo la chalinze limejipanga
kuhakikisha linawakamilishia maendeleo wananchi wake ili kuondoa changamoto
zote zilizokuwa zikiwakabili kwani serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na
Rais John Pombe Magufuli imekuwa ikifanya mambo yake kwa vitendo na wakati.
“Mheshiwa Makamu Wa Raisi, halmashauri yetu inajenga zahanati zaidi ya 12
ambazo ziko katika hatua za mwisho zikielekea kukamilika. Mheshimiwa Kikwete,
alizitaja baadhi ya Zahanati hizokuwa ni Chahua,Visakazi,Ubenazomozi,Pingo,Lulenge,
Magulumatale,Msigi, Mindukene,Mwetemo,Bago,Mandela na Dihozile” Alisema
Kikwete.
Aidha mbunge huyo aliongeza kuwa kuna vituo vya Afya ambavyo pia
vinaendelea kujengwa na serikali na vimekamilika kwa asilimia 90 mahususi kwa
sababu ya kusaidia masuala ya Wanawake na Watoto na zimepewa na uwezo wa
upasuaji ambavyo ni Kibindu, Miono, Lugoba, Chalinze na Msoga.Malengo yakiwa ni
kuondoa kabisa vifo vinavyotokana na kutopatikana kwa huduma bora za Afya hasa
kwa Wakina mama na Watoto katika jimbo la chalinze.
Mbunge huyo alitumia nafasi huyo kuwataka wananchi wa jimbo lake kutumia
fursa walizozipata za kuwa na wingi wa vituo vya afya kuhakikisha wanakwenda
kupatiwa matibabu katika sehemu zinazostahili na si kubaki majumbani na kupeana
tiba za kienyeji.
Naye mkuu wa mkoa Eng Evarist Ndikilo amemuhakikishia Makamu
wa Rais Mama Samia Suluhu kuwa halmashauri ya chalinze imekuwa kinara wa
utekelezaji wa miradi ya maendeleo kutokana na umoja wa viongozi wa eneo hilo.
Hivyo amempongeza mbunge wa jimbo hilo kwa jinsi anavyopambana na
ufanikishaji wa miradi ya maendeleo kwa kutumia wafadhili mbalimbali hivyo
wananchi wamtumie vizuri katika ufanikishaji wa maendeleo ya chalinze.
No comments:
Post a Comment