Thursday, October 25, 2018

SAMIA KUSHUGHULIKIA KERO ZA WAKAZI WA PANDE BAGAMOYO WANAOPISHA UJENZI WA BANDARI.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo kuhusu ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, katike la Mbegani kutoka kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) Mhandisi Karim Mattaka alipotembelea eneo hilo katika ziara yake ya kikazi mkoani Pwani.
...................................
WAKAZI wa Vijiji vya Pande na Mlingotini wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ambao wamehamishwa kupisha mradi wa bandari mpya ya Bagamoyo wameiomba serikali kuwasaidia kulipwa fidia na kuhamishiwa katika makazi mapya .

Akitoa kilio hicho kwa niaba ya wakazi wa maeneo hayo ,wakati makamu wa Rais Samia Suluhu alipokwenda eneo la Mbegani kutembelea ujenzi huo, mwenyekiti wa kitongoji cha Pande Muhsin Mneka alisema  walipangiwa kwenda eneo la Kitopeni na Kidagoni lakini wameshindwa kwenda kutokana fidia kutokamilika.

Alisema kuwa  baadhi ya watu walilipwa fidia lakini wengine hawajalipwa huku wengine wakiwa wamepunjwa fidia zao kwa kulipwa kidogo fedha ambazo hazitoshi kununulia maeneo mengine.

“Wapo waliolipwa hapa hadi laki moja, milioni tano na milioni moja kiasi ambacho hakikidhi, hatujakataa kupisha mradi ila makubaliano yetu hayajatekelezwa “alisema Mweka. 

Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Dk Shukuru Kawambwa alisema kuwa Kijiji hicho kina kaya 2,200 sawa na watu 16,500 ambao wanatakiwa kuhama eneo hilo.

Kawambwa alieleza, jambo hilo limekuwa ni changamoto kubwa hivyo kuna haja ya kuhakikisha suala hilo linafikia mwisho.

Akijibu hoja hizo,makamu wa Rais  Samia Suluhu alisema , suala hilo amelichukua na atalipeleka kwa Rais baada ya kukaa na mamlaka husika ,wizara ya ardhi, bandari na EPZA ili kulipatia ufumbuzi. 

Samia alifafanua malalamiko yote yatafanyiwa kazi na serikali haitadhulumu mtu haki yake.

Alisema kuhamisha watu hao ni fedha nyingi zinahitajika na kuna taarifa kuwa hata wale walioko eneo la Kitopeni na Kidagoni bado hawalipwa fidia zao .

Alifafanua apewa taarifa awali kuna watu 600 walipatiwa fidia ambazo hazikuwa haki zao ambazo zingesaidia kuwalipa waliostahiki. 

Samia aliwahakikishia serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama vinafuatilia wahusika hao ili kurejesha fedha hizo. 

Aliitaka halmashauri kuziweka fedha za fidia ya shule na zahanati zinazotolewa eneo hilo bila kutumia kwa matumizi mengine kwani inapaswa nguvu zao zibakie. 
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Mafunzo na Elimu ya Uvuvi (FETA) Yahya Mgawe kuhusu eneo ambalo litajengwa Bandari ya Bagamoyo.
Wanachi waliofika kumsikiliza Makamu wa Rais katika eneo la Chuo cha
Wakala wa Mafunzo na Elimu ya Uvuvi (FETA) ambako patajengwa Bandari ya Bagamoyo.

 
Mwenyekiti wa kitongoji cha Pande Muhsin Mneka akizungumza mbele ya Makamu wa Rais kuhusu kero za wananchi wa Pande na Mlingotini.
 
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Dk Shukuru Kawambwa, akizungumza mbele ya Makamuwa Rais Samia Suluhu Hassan.
 
Mkurugenzi wa Halmashuri ya Bagamoyo, Fatuma Latu akijbu hoja zilizowasilishwa upande wake.
 
Katibu tawala wa wilaya ya Bagamoyo, Hamza Amri Athumani akiwasikiliza madiwani wa viti maalum wa Halmashauri ya Bagamoyo, ambao ni Shumina Ismail Rashid wa kwanza kushoto, Hafsa Juma Kilingo wa kati na Togo Omari Hega katika eneo la Mbegani ambako Makamu wa Rais alifika kuagalia eneo linalotarajiwa kujenga Bandari ya Bagamoyo.
Wenyeviti wa Halmashauri, kulia ni Mwenyekiti wa Halmashuri ya Bagamoyo Ally Ally Issah na kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Saidi Zikatimu, katikati ni Diwani wa kata ya Zinga Mohamedi Mwinyigogo.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa meza kuu pamoja na viongozi waandamizi, wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa, wa tatu ni Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo na kutoka kushoto ni Naibu waziri wa Nishati, Subira Hamisi Mgalu, wa pili ni Naibu waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Atashasta Nditie na watatu ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo walipokuwa katika eneo la Mbegani Bagamoyo panapotarajiwa kujengwa Bandari ya Bagamoyo.

No comments:

Post a Comment