Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu akipokelewa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye
pia ni mbunge wa Mkuranga, Abdalla Ulega wakati alipowasili katika
eneo la kiwanda Mkuranga
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu akiongea na uongozi ,wafanyakazi na wageni mbalimbali
katika ziara hiyo
...................................
Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan, amefanya ziara katika kampuni ya
kutoka Ujerumani ya KNAUF inayotengeneza jasi (Gypsum) na vifaa vingine vya
kisasa vya ujenzi na kujionea uwekezaji inaoendelea kufanya wa kuzalisha bidhaa
bora za ujenzi katika kiwanda chake kilichopo eneo la Mkuranga mkoani Pwani.
Katika ziara hiyo ,Mh. Samia Suluhu Hassan,ambaye alikuwa katika ziara ya
kutembelea mkoa wa Pwani,alisema serikali itaendelea kujenga mazingira mazuri
ya uwekezaji ikiwemo kukabiliaana na changamoto ya umeme na kuwataka wawekezaji
kutangaza bidhaa zao ili watanzania wajue kuwa bidhaa walizozoea kununua nje ya
nchi sasa zinapatikana nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Bw.Zachopolous Georgions,alimweleza
Makamu wa Rais, aliyeongozana na viongozi mbalimbali wa serikali katika ziara
hiyo, kuwa hadi kufikia sasa kampuni tayari imewekeza zaidi ya shilingi bilioni
20/- na bado inaendelea kufanya uwekezaji, ili kuhakikisha bidhaa bora za
ujenzi zinazalishwa hapa nchini ili kukidhi ongezeko la masoko yaliyopo
sambamba na yaliyopo kwenye nchi jirani.
Bw. Georgions, alisema kampuni hiyo imewekeza katika biashara ya jasi
kanda ya Afrika Mashariki na imechagua, Tanzania kama makao yake makuu na
ilianza rasmi shughuli zake nchini miaka mitatu iliyopita na tayari imeweza
kuajiri watanzania kupitia uwekezaji wake.
Mkurugenzi alisema kwa sasa kampuni inatengeneza jasi kutokana na
mahitaji ya wateja wake na kwa kuanzia inatengeneza Gypsum zenye ukubwa wa
milimita tisa hadi 12 ambazo ni nzuri katika kukinga nyumba dhidi ya moto na
unyevu unaosababishwa na maji ya mvua.
“Tunatumia teknolojia mpya ya utengenezaji wa jasi ambayo inawezesha
matumizi ya chuma mahali ambako zamani zilikuwa zinawekwa mbao.
Teknolojia hiyo
tayari imeanza kutumika katika kiwanda cha Mkuranga pia tunatengeneza unga
maalumu wa jasi ambao unaweza kutumika kwenye ujenzi hata wa nyumba za gharama
nafuu”,alisema Georgions.
Aliongeza kusema kuwa KNAF Tanzania pia ina mradi maalumu wa kufundisha
vijana wa kitanzania kuhusu teknolojia mpya za ufungaji na utengenezaji wa jasi
na wanapohitimu wanapatiwa vyeti vinavyotambulika dunia nzima katika sekta ya
ujenzi vinavyowawezesha kufanya kazi katika nchi nyinginezo duniani.
KNAUF Tanzania, ni kampuni tanzu ya KNAUF yenye makao makuu Ujerumani,
ikiwa na maeneo ya uzalishaji na ofisi za mauzo 150 katika nchi zaidi ya 60
ikiwa imeajiri wafanyakazi 26,000 duniani kote.
Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni mbunge wa Mkuranga, Abdalla Ulega
akizungumza machache na Mkurugenzi Mtendaji wa KNAUF Gypsum Afrika Mashariki,
Zachopoulos Georgios.
Mkurugenzi
Mtendaji wa KNAUF Gypsum Afrika Mashariki, Zachopoulos Georgios akielezea
macheche kwa Makamu wa Rais juu ya kiwanda hicho.
Muonekano wa Eneo
la kiwanda hicho.
No comments:
Post a Comment