CHAMA Cha Mapinduzi CCM kimeshinda kwa kishindo
katika uchaguzi wa mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli mkoani hapa
baada ya aliyekuwa mgombea wa wa nafasi hiyo kwa tiketi ya CHADEMA Rita
Mona kujitoa kwenye kinyang’anyiro hicho.
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Licha ya Rita diwani wa kata ya Monduli Mjini Issac
Kopriano maarufu kwa jina la kadogoo alikuwa anawania nafasi hiyo kwa tiketi ya
CCM.
Pia makamu mwenyekiti ameshinda kwa kishindo baada
ya mpinzani wake Fadhili Mbwambo diwani wa kaya ya Majengo (CHADEMA)kujitoa
ukumbini wakati akiomba kura.
Baada ya wagombea hao wawili kujito kwenye
kinyang’anyiro hicho msimamizi wa uchaguzi huo ambaye pia ni mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya ya Monduli Steven Ulaya alisema kwa mujibu wa kanuni
lazima zipigwe kura za ndiyo na hapa.
Kufuatia agizo hilo madiwani wa 23 wa vyama vya
CHADEMA na CCM walipiga kura ambapo madiwani tisa wa CHADEMA walimpigia Kadogoo
kura za ndiyo na kuibuka na ushindi wa kishindo wa kura 23 kati ya kura zote 23
zilizopigwa.
Kwa upande wa nafasi ya makamu mwenyekiti wa
halmashauri CCM ilishinda kwa kishindo baada ya diwani wa kata ya
Naalarami Edward Lenanu kupata kura 22 kati ya kura 23 zilizopigwa baada
ya kura moja kuharibika.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi Kadogoo
aliishukuru CCM kwa kuendelea kumwamini na kumteua kugombea nafasi ya udiwani
kwenye uchaguzi mdogo wa marudio ambapo alipita bila kupingwa na kufanikiwa
kuwa diwani wa kata hiyo.
Kadogoo aliwataka wananchi,madiwani wa Monduli
pamoja na watumishi wa halmashauri ya Monduli kuweka tofauti zao pembeni na
kusimamia ajenda moja tuu ya maendeleo.
“Niwaombe wana Monduli wimbo wetu wa kila siku uwe
ni maendeleo popote tutakapokuwa ili tuweze kwenda na kasi ya rais Dk John
Magufuli ya kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo ya dhati”.
No comments:
Post a Comment