aziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola,
akionyesha moja ya nyumba ya askari wa Gereza la Mbigiri, Wilaya ya Mvomero,
Mkoa wa Morogoro, ambayo inahitaji matengenezo. Lugolo alifanya ziara ya
kushtukiza katika Gereza hilo la Kilimo kwa lengo la kupata kero na kuimarisha
uzalishaji wa kilimo na ufugaji. Kulia ni askari wa Gereza hilo, Sajenti
Lubimbi Sayi. Lugola alifanya kikao na askari na Maafisa wa Gereza hilo na
kuwataka kumpa kero zao bila kuwa na woga na hakuna atakaye wanyanyasa.
...........................................
Na Felix Mwagara, MOHA-Morogoro
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Kangi Lugola, amewataka askari pamoja na watumishi mbalimbali waliopo ndani ya
Wizara yake wawe huru kuuliza maswali, kusema kero zao zinazowakabili katika
vikao vyake na hakuna kiongozi yeyote atakaye wanyanyasa baada ya yeye
kuondoka.
Waziri Lugola amesema hayo baada ya
kuona baadhi ya watumishi katika ziara mbalimbali anazozifanya nchini, wanakua
na woga wa kusema kero zao wakihofia watapata matatizo baada ya yeye kumaliza
kikao.
, wakati anapata mambo mengi ambayo
yanamsaidia kutatua kero za watumishi wake licha ya kuwa baadhi ya watumishi
wanakua na woga wa kusema matatizo yanayowakabili.
Akizungumza katika kikao na askari na
Maafisa wa Jeshi la Magereza wa Gereza la Kilimo la Mbigiri, liliopo
Wami-Dakawa wilayani Mvomero mkoani Morogoro, jana, Lugola alisema ili aboreshe
utendaji kazi wa Wizara na Idara zake, anahitaji kujua matatizo mbalimbali ya
watumishi wake, hivyo katika kikao chake ruksa watumishi kuuliza maswali
kwasababu kupitia maswali hayo yanamsaidia sana kutatua kero zao.
“Mimi ndio Waziri wenu, ulizeni swali
lolote, toeni kero zenu na hakuna wakuwafuatilia baada ya kikao hiki, hiki ni
kikao cha Waziri wenu mmepata nafasi hii ulizeni, niambieni matatizo yenu
yanayowakabili ili tuyafanyie kazi,” alisema Lugola.
Pia aliwaambia watumishi hao endapo
watapata matatizo baada ya kusema kero zao katika kikao chake, wawe huru
kumuambia japo anaamini hakuna chochote kitakacho wakuta maana kikao chake
ambacho ni huru.
Lugola aliyasema hayo baada ya baadhi
ya askari wa Gereza hilo kuwa na hofu wakati walipokua wanauliza maswali ambapo
mmoja wao akitoa kero yake huku akitahadharisha kuwa Waziri huyo amlinde endapo
atapata matatizo mara baada ya kikao hicho kumalizika.
“Hivi huwa mnakua karibu na viongozi
wenu? Kwa mfano unakuta ukaribu huu wa kukaa hapa kwa kumkaribia Mkuu wa Gereza
katika kikao hiki ni wa leo tu kwasababu nipo, lakini baada ya kikao hiki
unakuta Mkuu wa Gereza au kiongozi yeyote mkubwa katika Jeshi hafikiwi na
askari, hii haiwezekani kuweni karibu na viongozi wenu, waambieni kero zenu na
pia nyie viongozi msiwatishe hawa askari wenu, sikilizeni kero zao,” alisema
Lugola.
Hata hivyo, Lugola aliutaka uongozi
wa Gereza hilo kuacha malalamiko na badala kutafuta majibu ya changamoto
zinazowakabili na pia wahakikishe wanasimamia nidhamu kwa askari na kutooneana,
na pia waendelee kutumia vitendea kazi vilivyopo katika Gereza hilo ili waweze
kuongeza uzalishaji katika shughuli mbalimbali za kilimo.
Kwa upande wake Mkuu wa Gereza hilo,
Kamishna Msaidizi wa Jeshi hilo, (ACP) Shija Fungwe, alimshukuru Waziri Lugola
kwa kufanya ziara katika Gereza lake, na pia maagizo yake aliyoyatoa
watayafanyia kazi likiwemo la kuongeza uzalishaji kupitia vitendea kazi
walivyonavyo na pia yeye pamoja na askari na Maafisa mbalimbali wa Gereza hilo
aliweka wazi kuwa wanaishi vizuri, kwa ushirikiano na pia wapo huru kuzungumza
naye kuhusu jambo lolote la utendaji kazi.
“Tunakushukuru sana Mheshimiwa Waziri
kwa kufanya ziara katika Gereza letu, tunakuahidi kufanyia kazi maagizo yako
uliotupa na pia tutaendelea kutumia vitendea kazi tulivyonavyo ili tuzidi
kuboresha, pamoja na kuimarisha uzalishaji wa Gereza hili,” alisema ACP Fungwe.
Waziri Lugola alifanya ziara ya
kushtukiza katika Gereza hilo ambalo linafanya shughuli za kilimo ya mazao
mbalimbali pamoja na ufugaji wa ng’ombe, kondoo, mbuzi na kuku ambapo kwa
ujumla wana mifugo zaidi ya 1000.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola,
akimsikikiliza Mkuu wa Gereza la Mbigiri, Mvomero, Mkoa wa Morogoro, Kamishna
Msaidizi wa Magereza, (ACP) Shija Fungwe (kulia) alipokua anatoa taarifa ya
utendaji kazi wa Gereza hilo la Kilimo. Lugola alifanya ziara ya kushtukiza
katika Gereza hilo kwa lengo la kupata kero na kuimarisha uzalishaji wa kilimo
na ufugaji. Lugola pia alifanya kikao na askari na Maafisa wa Gereza hilo na
kuwataka kumpa kero zao bila kuwa na woga na hakuna atakaye wanyanyasa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola,
akizungumza na askari na Maafisa wa Magereza wa Gereza la Kilimo la Mbigiri
lililopo Mvomero, Mkoani wa Morogoro, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza
katika Gereza hilo kwa lengo la kupata kero na kuimarisha uzalishaji wa kilimo
na ufugaji. Kushoto kwa Waziri huyo ni Mkuu wa Gereza hilo, Kamishna Msaidizi
wa Magereza, (ACP) Shija Fungwe. Lugola aliwataka na askari na Maafisa
hao kusema kero zao bila kuwa na woga na hakuna atakaye wanyanyasa.
No comments:
Post a Comment