Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Kassim Majaliwa jana Novemba 3, 2018, amefunga wiki ya maonesho ya viwanda
Kibaha, Mkoani Pwani, yaliyokuwa yakifanyika kwenye viwanja vya CCM-Sabasaba,
eneo la Picha ya Ndege.
........................................
NA OWM, PWANI
WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka Wizara zinazohusika na masuala ya viwanda, Ofisi
za Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na sekta
binafsi watambue na waondoe vikwazo na urasimu dhidi ya ujenzi na ustawi wa
viwanda nchini.
Pia,
Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles
Mwijage ampelekee taarifa ya hatua iliyofikiwa juu ya kampuni ya Budget Motors
walioomba kibali cha kutengeneza na kuunganisha bodi za mabasi tangu mwaka jana
na hawajajibiwa.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Novemba 3, 2018) wakati akifunga wiki ya
maonesho ya viwanda yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Sabasaba katika kata ya
Picha ya Ndege, Kibaha mkoani Pwani. Amesena uwepo wa viwanda nchini unatoa
ajira nyingi.
“Serikali
ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeamua kujenga uchumi
wa viwanda utakaokuwa mhimili mkuu wa maendeleo ya Taifa na wananchi, hivyo
itaendelea kutoa ushirikiano ili kuhakikisha ajenda ya ujenzi wa viwanda
inafanikiwa.”
Alisema
katika kupunguza vikwazo na kuboresha sera nchini, Rais Dkt. Magufuli ameweka
msukumo wa kutosha ili kurahisisha na kuondoa ukiritimba kwenye shughuli zote
za kibiashara, lakini pia katika kuboresha sera za Taifa za kodi ili kulinda
viwanda vya ndani
Waziri
Mkuu amesema umuhimu wa viwanda umetokana na Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/2020 ambayo inaielekeza Serikali kuweka nguvu
katika ujenzi wa viwanda ili kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya
mwaka 2025.
Alisema
kwa msingi huo, Rais Dkt. Magufuli alitoa msukumo wa sekta binafsi nchini
kuanzisha viwanda vinavyotumia malighafi zinazozalishwa nchini kutokana na
mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na maliasili, vikiwemo viwanda vya nguo, sabuni,
korosho na matunda.
Waziri
Mkuu ameongeza kuwa uwepo wa viwanda nchini utasaidia kuongeza wigo wa mapato
ya Serikali kupitia kodi na tozo mbalimbali. “Huu ndio mwelekeo wa Serikali ya
awamu ya tano unaolenga kuifikisha nchi kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka
2025.”
Kuhusu
suala la kampuni ya Budget Motors, Wiziri Mkuu amesema ifikapo Ijimaa (Novemba
9, 2018) Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji awasilishe taarifa kuhusu
suala hilo la kibali. “Huu ni urasimu, ni bora apewe atengeneze na akikosea
arekebishwe.”
Kampuni
ya Budget Motors inadai kuwa iliomba kibali cha kuwa na uthibitisho wa
kutengeneza na kuunganisha bodi za mabasi kutoka Shirika la Viwango Tanzania
(TBS), kwa takribani mwaka mmoja bila ya kujibiwa. Walitoa malalamiko hayo kwa
Waziri Mkuu alipotembelea banda.
Katika hatua nyingine,
Waziri Mkuu ametoa rai kwa taasisi zenye miradi mbalimbali nchini pamoja na
wananchi kuthamini na kuzitumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya hapa
nchini zikiwemo na za viwanda vya mkoa wa Pwani kwani zina viwango vya ubora.
“Wakati
natembelea mabanda kwenye maonesho haya nimeshuhudia bidhaa nyingi nzuri na
zenye ubora. Nimeona wazalishaji wa saruji, mabati, nondo, marumaru, mabomba ya
plastiki, chuma, zana za kilimo, vyakula, vinywaji na vifungashio.”
Waziri
Mkuu amesema kupitia maonesho hayo ya viwanda vilivyopo katika mkoa wa Pwani
vimeudhihirishia umma kuwa vina uwezo mkubwa wa kuzalisha bidhaa zilizo bora na
hata kuzidi zile zinazoingizwa kutoka nje, amewahamasisha wananchi kutumia
bidhaa za ndani.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo ameiagiza mikoa yote nchini kuhakikisha inatumia
bidhaa zinatengenezwa na viwanda vya ndani katika miradi mbalimbali ya ujenzi
wanayoitekeleza kama ujenzi wa hospitali za wilaya na vituo vya afya.
Amesema
Wakuu wa Mikoa ni lazima wahakikishe bidhaa kama saruji, nondo, marumaru,
mabati zinavyotumika katika ujenzi ziwe vimezalishwa na viwanda vya ndani kwa
sababu vina viwango vya ubora unaotakiwa na pia itasaidia kuondoa tatizo la
soko la bidhaa hizo.
Naye,Waziri Mwijage amewataka
watendaji wanaohusika na masuala ya viwanda kutoweka vikwazo kwa wawekezaji
ambao wanakwenda katika ofisi zao kwa ajili ya kutafuta maeneo ya kuwekeza
kwenye viwanda au wanaohitaji vibali kwani jambo hilo halina tija.
Moanesho
hayo yaliyofunguliwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Oktoba 29,
2018, yalilenga kuwakutanisha wazalishaji bidhaa za wviwanda na wanunuzi
(masoko), ambapo pia taasisi za serikali zinazohusika na utoaji huduma
mbalimbali zilishiriki pia.
Miongoni
mwa taasisi hizo, ni Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi WCF, ambao kazi yake kubwa
ni kutoa Fidia kwa wafanyaklazi walioumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi.
Moja ya
ujumbe mkubwa alioutoa siku anafungua maonesho hayo kwa waajiri kote nchini,
Makamu wa Rais aliuagiza
uongozi wa (WCF), kuendelea kuwafuatilia waajiri ambao bado hawajajisajili ili waweze kufanya hivyo.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa,
(kushoto), akimkabidhi cheti cha shukrani Kaimu Meneja
Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Semu Mwakyanjala mwishoni mwa maonesho hayo
Novemba 3, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Bibi
Florence Max Mambali wakati alipotembelea banda la Kampuni ya kufuga
kuku na kuzalisha vifaranga vya kuku ya Mkuza Chicks katika
Maonesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba
uliopo katika eneo la Picha ya Ndege, Kibaha, Novemba 3, 2018. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Mawaziri na
viongozi wengine wa juu serikalini, wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi
na wawakilishi wa taasisi za umma na binafsi waliowezesha kufanyika kwa
maonesho hayo.
No comments:
Post a Comment