Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumz jambo na Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba katika
mkutano aliouhutubia kwenye kijiji cha Mponde wilayani Lushoto, Novemba 1,
2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
.........................................................
SERIKALI imemaliza mgogoro uliodumu kwa miaka mingi kati ya
wakulima wa chai wa wilaya za Lushoto na Korogwe na kampuni ya Mponde Tea
Estate uliosababisha kufungwa kwa kiwanda cha chai cha Mponde baada ya kuagiza
kiwanda hicho kianze kazi.
“Waziri Mwijage na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilomo Prof. Siza Tumbo
hakikisheni kazi ya kukagua kiwanda na mitambo inafanyika haraka na kubaini
mitambo ipi ni mizima na ipi ina hitilafu ili ukarabati ufanyike na kiwanda
kianze kazi mara moja.”
Uamuzi huo wa Serikali umetangazwa leo (Alhamisi, Novemba 1, 2018) na Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye kijiji cha Kweminyasa kata ya Mponde, wilayani Lushoto baada
ya kutembelea kiwanda hicho .
Waziri Mkuu amesema mwaka 1999 Serikali iliamua kuwapa wakulima wa chai
na kiwanda hicho kwa ajili kuwawezesha kuwa na sehemu ya kuchakata
chai yao lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kiuchumi. Imeamua kukirudisha
Serikali baada ya kuwepo migogoro iliyoathiri uzalishaji kiwandani hapo.
Kuhusu suala la madeni ya watumishi, ameagiza watafutwe na madai
yaorodheshwe kwa ajili ya malipo, amewahakikisha wananchi hao kuwa suala la
ajira ambazo zilipotea baada ya kiwanda kufungwa zitarudi kwa sababu Serikali
inataka kuona kiwanda kikifanya kazi.
“Serikali imeamua kukichukua kiwanda hiki ambacho awali ilikikabidhi
wakulima wa chai na kwamba itahakikisha lengo lake la kuboresh kilimo
linafanikiwa na wakulima wanaendelea kulima zao la chai. Hatutaki
kusikia masuala ya Utega wala Mponde hapa si mahali pake.”
Amesema wakulima hao walikosea kwa kuunda Umoja wa Wakulima wa Chai
(UTEGA) ambapo katika kusajili badala ya kuanzisha ushirika wao walisajili NGO
ambayo ilikuwa na wanachama wake, huku kiwanda kikiwa kimeanzishwa kwa ajili ya
wakulima wote, jambo ambalo lilisababisha mgogoro baina ya wakulima na viongozi
wa UTEGA.
Waziri Mkuu ameongeza kuwa wakati mgogoro huo ukiendelea kati ya UTEGA na
wakulima wa chai wasiokuwa wanachama wa NGO hiyo, uliibuka mgogoro mwingine
baina ya wakulima wote pamoja na muwekezaji ambaye ni kampuni ya Mponde Tea
Estate baada ya kukabidhiwa kiwanda hicho na uongozi wa UTEGA bila
ya wao kushirikishwa.
Amewasisitiza wakulima wafufue mashamba yao kiwanda ni
cha Serikali hivyo watakuwa wamepata sehemu ya uhakikika
ya kupeleka chai ambayo itachakatwa. Pia ameagiza Mrajisi wa Ushirika aende kwa
wakulima na kutambua idadi yao pamoja na kujua ukubwa wa mashamba yao.
Amesema baada ya kubaini idadi ya wakulima na ukubwa wa mashamba yao
awasaidie katika kuunda vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kisha kuunda
ushirikia wao ambao watautumia katika kusimamia zao lao la chai na kuhakikisha
mkulima ananufaika.
Waziri Mkuu amesema zao la chai ni miongoni mwa mazao makuu sita ya
kimkakati, mengine ni korosho, kahawa, tumbaku, pamba na chikichi, hivyo
amewataka wafufue mashamba yao na waendelee kuiamini Serikali yao ambayo
imejidhatiti kuwahudumia.
Awali,Waziri wa Nchi Ofisi ya Makam wa Rais Muungano na Mazingira,
January Makamba alisma Mgogoro huo wa kiwanda cha Mponde ulianza tangu mwaka
1999 na ilipofika mwezi Mei 2013, wananchi walimlalamikia kwa kushindwa kutatua
tatizo hilo.
Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli aliwaomba wananchi hao waendelee
kuwa na subira wakati suala lao likiwa linaendelea kushughuliwa na Serikali. “Mgogoro
huo umesababaisha kudhorota kwa uchumi kwa sababu wananchi wengi waliacha
kulima chai baada ya kiwanda hicho kufungwa miaka mitano iliyopita.”
Hivyo Makamba ameiomba Serikali iwasaidie wakulima wa zao la chai kuwapa
miche mipya pamoja na pembe jeo kwa ajili ya kufufua zao hilo na kukiwezesha
kiwanda cha chai MPonde kupata malighafi kama ilivyokuwa hapo awali.
Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles
Mwijage alisema kuwa tayari amekuja na wataalam kwa ajili ya kukagua
mashine zote zilizopo kiwandani hapo ili mchakato wa kukiwasha
uanze mara moja.
Mwijage alisema “mimi kama Waziri mwenye dhamana ya viwanda nawaambia
wananchi muondoe wasiwasi tayari kiwanda kimeshafunguliwa maana sitaondoka hapa
Bumbuli mpaka kieleweke.”
Wananchi
wakimpungia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasili kwenye
kijiji cha Mponde wilayani Lushoto kukagua kiwanda cha chai cha Mponde na
kuzungumza na wananchi, Novemba 1, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment