Mkurugenzi Mkurugenzi wa
Uhamasishaji na Uwekezaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania John Mnali
...............................................................
Na Grace Semfuko-MAELEZO
Tanzania imepokea wawekezaji kutoka Jimbo la Guangzhou Nchini China
watakaokuja kuwekeza nchini kwenye eneo la ukanda wa uwekezaji la Kilua
lililopo Kibaha Mkoani Pwani ambao watawekeza kwenye viwanda vya ngozi kwa
ajili ya kutengeneza bidhaa mbalimbali.
Akizungumzia ujio huo wa wawekezaji wa China Mkurugenzi Mkurugenzi wa
Uhamasishaji na Uwekezaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania John Mnali amesema
kwa awamu ya kwanza wawekezaji hao wametenda Dola milioni mia moja ikiwa ni
kiwango cha kuanzia kwa awamu ya kwanza ya uwekezaji huo.
“Tumepokea wawekezaji hawa ambao wanakuja kuwekeza nchini kwa awamu ya
kwanza kiwango cha kuanzia ni dola milioni 100, huu sio uwekezaji Mdogo ni
uwekezaji Mkubwa sana, hizi ni juhudi za Mohammed Kilua kwa kushirikiana na
TIC” alisema John Mnali Mkurugenzi wa Uhamasishaji na uwekezaji wa TIC.
Mnali alisema wamekuwa wakihamasisha uwekezaji kwenye mataifa mbalimbali
Duniani hivyo ujio wa Raia hao wa China ni faraja kubwa kwa Serikali ya
Tanzania na hasa katika awamu hii ya Serikali ya Rais Magufuli ya uchumi wa
viwanda.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa eneo la uwekezaji la Kilua lililopo Kibaha
Mkoani Pwani Bw.Mohammed Kilua amesema pamoja na ujenzi wa viwanda vya ngozi za
wanyama kwa ajili ya utengenezaji wa bidhaa mbalimbali lakini pia wawekezaji
hao wameonyesha nia ya kuwekeza kwenye viwanda vya ubanguaji wa korosho pamoja
na kilimo cha zao hilo
“ Hawa wawekezaji Kutoka Nchini China pia wameonyesha nia ya kuwekeza
kwenye Korosho, na wiki tatu zijazo tutawapeleka Mtwara kuangalia maeneo ya
kuwekeza ili waweze kuangalia namna ya kuwekeza” alisema Mohammed Kilua
No comments:
Post a Comment