MTANGAZAJI maarufu wa Habari wa Kituo cha Runinga cha Star Tv na Radio
Free Africa, (Sahara Media Group) ambaye pia alikuwa mkongwe kwenye tasnia
hiyo, Samadu Hassan amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, nyumbani kwake eneo
la Miembe Mitatu, jirani na kituo cha Chakechake wilayani Nyamagana jijini
Mwanza.
Mdogo wa Samadu, Latifa Hassan amesema kaka yake alikuwa akisumbuliwa na
kifua kwa zaidi ya wiki moja, kabla ya kufikwa na umauti.
“Jana jioni, Samadu alirudi nyumbani kwake akitokea kazini alikuwa mzima
wa afya, lakini alikuwa akidai kifua kinamsumbua.
Tulikula naye pamoja chakula
cha jioni, akadai kifua kinamsumbua, tulimwambia twende hospitali ili
akatibiwe, lakini alisema atakwenda kesho (leo).”
“Ilipofika saa sita kasoro usiku, ghafla hali yake ikabadilika na
kuanguka chini na kuanza kutokwa na mapovu mdomoni. Tulikimbia kwenda kutafuta
gari kumuwahisha hospitali, hadi tunapata gari na kurudi ndani, tulikuta tayari
ameshaaga dunia,” amesema Latifa.
No comments:
Post a Comment