Mkuu
wa Mafunzo na Operesheni (JWTZ) Meja Jenerali Alfred Fabian Kapinga
akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Mkuu ya Jeshi la Wananchi
Upanga jijini Dar es salaam wakati alipotangaza kufamyika kwa mazoezi ya
pamoja kwa nchi za Afrika Mashariki yatakayofanyika mkoani Tanga mwezi ujao,
Kushoto ni Kanali Martin Msumali Naibu Mkurugenzi wa Mafunzo Makao Makuu ya
Jeshi.
Mkuu
wa Mafunzo na Operesheni (JWTZ) Meja Jenerali Alfred Fabian Kapinga
akifafanua zaidi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mazoezi
ya kijeshi yatakayofanyika mkoani Tanga na kushirikisha majeshi ya nchi za
Afrika Mashariki kushoto ni Kanali Martin Msumari Naibu Mkurugenzi wa Mafunzo
Makao Makuu ya Jeshi na kulia ni Meja Gaudence Ilonda Kaimu Mkurugenzi wa
habari na Uhusiano (JWTZ)
.................................................
JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanatarajia kuwa wenyeji
wa zoezi la mafunzo yaitwayo Ushirikiano imara 2018 litakaloshirikisha nchi za
Afrika Mashariki zikiwemo Burundi, Rwanda, Kenya na Uganda ambapo mafunzo
yataendeshwa mkoani Tanga .
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam Mkuu wa Mafunzo na
Operesheni (JWTZ) Meja Jenerali Alfred Fabian Kapinga amesema kuwa, zoezi
hilo ni la medani na litafanyika katika wilaya za mijini pamoja na Wilaya ya
Muheza mkoani Tanga.
Ameeleza kuwa zoezi hilo litaanza rasmi tarehe 05 mpaka 21, sambamba na
hilo mafunzo hayo yatalenga kujenga uwezo wa kukabiliana na uhalifu pamoja na
majanga.
Pia amesema kuwa dhumuni la zoezi hilo kikanda ni kubadilishana uzoefu wa
kiutendaji, kuimarisha mahusiano baina ya nchi, majeshi ya Afrika Mashariki
pamoja na taasisi zingine za kiraia ambazo zitashiriki zoezi hilo.
Sanjari na hilo kutakuwa na kazi za kusaidia jamii katika shughuli
mbalimbali zikiwemo ujenzi wa madarasa, ofisi za walimu pamoja na vyoo katika
Shule ya msingi ya Machemba iliyopo Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, pia kutakuwa
na utoaji wa huduma za tiba kwa wananchi katika eneo la zoezi.
Hivyo, Meja Fabian ametoa rai kwa wakazi wa Tanga kuonyesha ukarimu
pamoja na amani baina ya wageni watakaokua kwa kipindi chote cha mafunzo kama
walivoonyesha mwaka jana ambapo mafunzo yalikua yakiendeshwa.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mafunzo na Operesheni (JWTZ) Meja
Jenerali Alfred Fabian Kapinga.
No comments:
Post a Comment