MKUU
wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama akizungumza na waandishi wa habari
, wakati akitolea ufafanuzi masuala mawili ambayo makamu wa Rais Samia Suluhu
aliyagusia kwenye ziara yake aliyoifanya wilayani humo,mwishoni mwa wiki
iliyopita.
.................................................
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
MKUU wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama, atolea ufafanuzi
juu ya hatua ya makamu wa Rais ,Samia Suluhu ,kukataa kuzindua stendi mpya ya
Mailmoja ambapo amesema yeye alishaweka hofu kuupokea mradi huo tangu kipindi
cha nyuma “;na mhandisi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ndio aliyewafikisha
hapo.
Aidha amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Kibaha Vijijini
,kumsimamisha cheo ofisa manunuzi na ugavi, Peter Mboje kwa madai ya kutumia
vibaya ofisi yake kujipatia fedha kinyume na utaratibu.
Aliyasema hayo kwa waandishi wa habari , wakati akitolea ufafanuzi
masuala ambayo Samia aliyagusia kwenye ziara yake aliyoifanya wilayani
humo,mwishoni mwa wiki iliyopita.
Assumpter alisema yeye anaungana na makamu wa Rais kujiridhisha kwanza na
uchunguzi.
Alisema alishakataa utekelezaji wa mradi huo na kuomba usipitiwe
kuzinduliwa kwakuwa una baadhi ya kasoro na hauendani na thamani ya bilioni 3.2
Assumpter alibainisha,kutokana na hofu hiyo na malalamiko kutoka kwa
wananchi alihitaji apatiwe ripoti ya gharama za ujenzi ambayo mhandisi wa mji
huo alikaidi na hajampatia hadi sasa .
“Nilimwambia alikaidi, sina mamlaka ya kumfanya chochote ,acha
tuone uchunguzi unaleta majibu yapi ili kujiridhisha na kuondoa minong’ono kwa
wananchi ”
“Serikali hii ni sikivu ,ukiona wananchi wanasema sema inabidi kufanyia
kazi suala wanalolalamikia ,tusipuuzie minong’ono ya watu kikubwa tuwe
tunaifanyia kazi “alisema Assumpter.
Alitoa wito kwa wakurugenzi wa halmashauri zote hizo mbili, wakipewa
ushauri wausikilize na wafanye nae kazi kama timu moja.
Akizungumzia sakata la ofisa manunuzi ,alisema , anaviachia vyombo vyake
vya ulinzi na usalama kuchunguza juu ya tuhuma zinazomkabili mtumishi huyo
ndani ya siku 14 kuanzia sasa.
Assumpter alieleza ,ofisi yake imefuatilia na kupata ushahidi wa watu
watano wa awali ndipo ameamua kuchukua maamuzi hayo.
Alielezea ,Mboje anadaiwa kutumia nafasi yake kuomba fedha kwa
wakandarasi wa ujenzi wa mradi wa upanuzi wa kituo cha afya Mlandizi
,akiwadanganya ametumwa fedha na mkurugenzi wa halmashauri ,hali inayosababisha
kusuasua kwa mradi.
“Hakuna haja ya kumsubiri Samia ,nimefuatilia na kubaini ametumia
madaraka yake vibaya ,” Mfano tumepata taarifa zake anasumbua mjenzi wa jengo
la OPD na fundi wa jengo la upasuaji”alifafanua Assumpter .
Assumpter alisema ,uchunguzi ukikamilika na kubaini ametenda kosa hilo
,sheria itachukua mkondo wake.
No comments:
Post a Comment