Mkuu
wa kanda ya Mashariki (TCRA) Lawi Odiero akizungumza.kwenye maonyesho hayo.
..........................................
NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeshawachukulia hatua za kisheria
watu nane wanaodaiwa kukiuka sheria za mtandao, ikiwemo kusambaza picha za nusu
uchi, video za ngono na kutupia matusi katika kipindi cha July -Septemba mwaka
huu.
Aidha wito umetolewa kwa jamii kuacha matumizi mabaya ya mitandao ya
kijamii ikiwa ni pamoja na video za ngono kwani kwa kufanya hivyo
hawatamuangalia mtu kwa sura ama umaarufu bali sheria itachukua mkondo
wake.
Ofisa mkuu wa mawasiliano kwa umma (TCRA) Semu Mwakyanjala
aliwatahadharisha ,watu wasisambaze picha ama video za ngono na kuanzisha
tovuti hizo kwani ni kukiuka sheria.
Alieleza kuna faida unapotumia mtandao inarahisisha mawasiliano
,unapunguza gharama ,inaokoa muda ,inatoa elimu na kukuza biashara badala ya
kutumia masuala yasiyo na tija.
“Kwasasa hatuna masihala, tunashirikiana na jeshi la polisi kubaini wale wanaokaidi
kufuata sheria zilizopo “alieleza Mwakyanjala.
Aliiomba jamii kutunza vifaa vya kielektronik ili watu waeiibe na kutymia
vibaya .
Nae mkuu wa kanda ya Mashariki (TCRA) Lawi Odiero alisema, sheria ya
kielektroniki iliyopo inakataza kusambaza ngono na baadhi ya watu wanachukuliwa
hatua ya kulipa faini sh. mil tano ama miaka mitatu jela.
Aliwaasa wananchi kwenda kutembelea banda lao kujifunza ili kuelewa
sheria zinazowabana ili kuepukana na adhabu.
Odiero alieleza wazingatie wasiweke namba za siri kwenye simu ama
internet miaka ya kuzaliwa bali watumie maneno mengine kwani sio rahisi
kughushi.
Akizungumzia ving’amuzi alisema ,serikali kupitia TCRA iliondoa baadhi ya
channel kwenye baadhi ya visimbuzi.
Odiero alifafanua, Azam, Dstv na Zuku huduma wanatoa kwa kulipisha hivyo
hawaruhusiwi kubeba channel za ndani.
Watumiaji wa internet hadi sasa nchini wapo milioni 22 ,luninga
zipo 34 ,vituo vya redio zaidi ya 150 kutoka kituo kimoja kilichokuwepo mwaka
1961.
No comments:
Post a Comment