Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi
Hamad Masauni akizungumza katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Stendi
ya Mabasi wilayani Newala leo, ambapo ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata
Viongozi wa Vyama Vya Msingi vya Ushirika ambao wametoroka na fedha za wakulima
wa korosho wilayani hapo,Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Newala Aziza Mangosongo.
Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mwananchi wa Newala,Shadrack Ntesi akimuuliza
swali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(hayupo
pichani), wakati wa Mkutano wa Hadhara uliofanyika leo katika Stendi ya Mabasi
wilayani hapo.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi
Hamad Masauni akisalimiana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya
ya Newala baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi,Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo
Aziza Mangosongo.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
..............................
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara
kuwakamata Viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika wanaotuhumiwa
kukimbia na Kiasi cha Shilingi Bilioni 1.2/= za wakulima ambazo ni
madeni ya Korosho.
Ametoa kauli hiyo leo wakati
akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Newala katika Mkutano wa
Hadhara uliofanyika Viwanja vya Stendi Kuu baada ya kupokea Ripoti ya Jumla ya
Madeni wanayodai wakulima katika Wilaya za Mtwara, Masasi, Nanyumbu, Newala na
Tandahimba.
“Nilivyofika hapa Mtwara jambo la
kwanza lilikuwa kumuuliza Kamanda wa Polisi wa hapa juu ya utekelezaji wa agizo
la Mheshimiwa Rais alilolitoa siku za hivi karibuni alipokuwa ziara na kuagiza
kukamatwa kwa viongozi wawili wa vyama vya msingi
vya ushirika wanaodaiwa fedha za korosho na wakulima,
ameniambia walitekeleza agizo na hao viongozi wawili tayari wameanza
kulipa hizo fedha,” amesema Masauni.
Akizungumza baada ya kupokea ripoti
ya madeni kwa Wilaya zote za Mkoa wa Mtwara Naibu Waziri Masauni amelitaka
Jeshi la Polisi kuwakamata viongozi wengine katika wilaya zilizobakia za
Mtwara, Newala, Masasi, Nanyumbu na Tandahimba ambazo katika taarifa ya jumla
ya mkoa inaonyesha takribani Shilingi Bilioni 1.2 bado zinadaiwa na wakulima
hao kutoka kwa viongozi wa vyama hivyo.
“Mheshimiwa Rais kwenye ziara yake
aliishia wilaya ya Masasi lakini katika ripoti hapa inaonyesha katika wilaya
zingine wakulima pia wanadai fedha zao ambacho ni kiasi kikubwa,nakuagiza
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara kuwakamata viongozi wengine katika wilaya
zilizobakia na hakikisha kiasi hicho cha fedha cha wakulima hao kinalipwa,”
amesema Masauni.
Katika taarifa hiyo iliyotolewa na
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara,Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Blasius Chitanda
inaonyesha jumla ya Vyama vya Ushirika 61 bado vinadaiwa na wakulima katika
wilaya za Mtwara, Masasi, Tandahimba na Newala kuanzia Msimu wa Korosho wa
Mwaka 2015/2016 hadi 2017/2018.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
katika mkutano huo baadhi ya wakulima wanaodai fedha zao waliiomba serikali
kuhakikisha wanalipwa haki yao kwani madeni hayo yamechukua muda mrefu hali
inayopelekea kuzorotesha shughuli zao za kuchumi huku familia zao zikipata
taabu kutokana na fedha zao kutopatikana kwa wakati.
No comments:
Post a Comment