Moja
ya shamba darasa katika eneo la Ziwa Ikimba.
......................................
Na
Alodia Dominick, Bukoba.
Wakulima
wapatao 5,000 wanatarajiwa kufikiwa katika mradi wa kilimo bora cha migomba
katika kata zilizopo kandokando ya ziwa Ikimba katika halmashauri ya Bukoba
vijjini.
Afisa
ugani Deusdedith Rweyemamu anayesimamia eneo la Ziwa Ikimba amesema kuwa mradi
huo umeanza Februari mwaka huu na kwamba lengo la mradi ni kuongeza ubora
katika zao la mgomba.
Rweyemamu
amezitaja, kata zenye mradi huo kuwa ni Kata ya Izimbya, Rubale, Kaibanja,
Kyamulaile, Ruhunga, Kikomero na Buterankuzi.
Aidha,
ameongeza kwa kusema kuwa, katika kata ya Buterankuzi kuna mashamba darasa 27,
ambayo husaidia wakulima kwenda kujifunza kilimo bora cha migomba na kisha
kwenda kuboresha mashamba yao.
Baadhi
ya wakulima ambao wako katika mradi huo wamesema kabla ya mradi huo migomba yao
ilikuwa inastawisha chane mbili za ndizi lakini kwa sasa kutokana na elimu
waliyoipata tayari wameanza kustawisha migomba mizuri ambayo wanatarajia itakuwa
na chane kuanzia kumi na kuendelea.
Mradi
huo wa ustawishaji wa migomba bora unasimamiwa na shirika la Matumaini Mapya
lililopo Bukoba kupitia mradi wa life long learning for farmers (L3F) kwa
kushirikiana na kituo cha utafiti Maruku
No comments:
Post a Comment