Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa,
Mzee Ally Mkongea akizungumza katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru wilayani
Ruangwa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Nangumbu wilayani
humo, Oktoba 9, 2019, kushoto ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Kulia ni Mkuu
wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa.
.....................................
Na
Hdija Hassan, Lindi.
Kiongozi
wa mbio za Mwenge wa uhuru Mzee Mkongea Ally amewataka Watanzania waliokuwa na
sifa ya kupiga Kura kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye dafutari la
kupiga kura ili waweza kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi wa Serikali za
mitaa.
Mkongea
ametoa wito huo alipokuwa akitoa ujumbe wa Mwenge wa uhuru kitaifa katika
kijiji cha Nangumbu Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi kwa wananchi
wa Wilaya hiyo.
Uchaguzi
huo unaotarajiwa kufanyika November 24 utahusisha wenyeviti wa mitaa, vijiji,
vitongoji, wajumbe wa Halmashauri kuu na wajumbe wa Viti maalumu.
Mzee
alisema swala la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni suala la kikatiba na kisheria
kwamba ni haki ya kila mwananchi aliekuwa na sifa kushiriki katika Uchaguzi huo.
"Serikali
za mitaa zinatambulika kutokana na Katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania
ya Mwaka 1977 , Serikali za mitaa zimekuwa zikifanya Kazi muhimu Sana katika
maeneo yetu ikiwemo kushajihisha shughuli za maendeleo, kuhamasisha Wananchi
kutunza mazingira, pamoja na kuhakikisha Wananchi wanaishi katika hali ya
usalama na amani" Alisema Mkongea.
Awali
akiwasalimia wananchi, Mbunge wa Jimbo hilo la Ruangwa ambae pia ni Waziri Mkuu
wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, Alitumia fursa hiyo kutoa
taarifa ya wananchi waliojitokeza kujiandikisha katika dafutari la kupigia kura
katika Wilaya hiyo ya Ruangwa Ambapo alisema kuwa kwa siku ya Tarehe 8 Pekee
jumla ya wananchi 28 elfu waliojitokeza kujiandikisha.
Pamoja
na mambo mengine Majaliwa pia, aliwataka wananchi ambao wanasifa za kugombea nafasi
mbalimbali za uongozi kujitokeza kugombea pamoja na kuwataka kuwaasa wapiga
Kura kuchagua viongozi Bora, wachapa Kazi na waadilifu.
No comments:
Post a Comment