Tuesday, October 1, 2019

MAAFISA WA POLISI WAMALIZA ZIARA YA MIRADI YA SERIKALI

Kamishna wa Utumishi na Rasilimali Watu CP Benedict Wakulyamba akizungumza na Meneja wa Mradi wa Treni ya Mwendo Kasi kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro wa Kampuni ya Yapi Markezi, wakati wa ziara ya Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika mradi huo.

Mhandisi Lulu Levira wa Daraja jipya la Salender akitoa maelezo kwa Maafisa Wakuu Waandamizi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi walipotembelea Mradi huo unaoendelea na ujenzi. Picha na Jeshi la Polisi.

Mhandisi Machibya Masanja wa Shirika la Reli Tanzania na Meneja wa Mradi wa Treni ya Mwendo kasi awamu ya kwanza akitoa maelezo kwa Maafisa Wakuu Waandamizi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi walipotembelea Mradi huo unaoendelea na ujenzi.

Meneja wa Mradi wa Treni ya Mwendo Kasi kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro wa Kampuni ya Yapi Markezi Abdullah, akitoa maelezo ya mradi huo kwa Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi wakati wa ziara ya Maafisa hao katika mradi huo unaoendelea na ujenzi. 

Katikati ni Kamishna wa Utumishi na Rasilimali Watu CP Benedict Wakulyamba na kulia ni Mhandisi Machibya Masanja wa Shirika la Reli Tanzania na Meneja wa Mradi wa Treni ya Mwendo kasi awamu ya kwanza. 

Picha na Jeshi la Polisi.

No comments:

Post a Comment