Tuesday, October 1, 2019

MWENYEKITI UVCCM PWANI ATEULIWA KUWA DAS WILAYA YA ILALA.




Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais , Ikulu imefafanua kuwa, aliyehamishwa kituo cha kazi kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na kwenda kuwa Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya itigi Mkoani Singida ni bw. John Kulwa Magalula.

Uhamisho huo umefanywa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 01 Oktoba 2019 .

aidha, aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala ni Bi Charangwa Selemani Magwiro.

Uteuzi huo umefanywa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapteni Mstaafu George Mkuchika kuanzia leo tarehe 01 Oktoba 2019.


 Aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa pwani, Bi Charangwa Selemani Magwiro, akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru siku ya makabidhiano kati ya Mkowa wa Pwani na Morogoro.

   Bi Charangwa Selemani Magwiro, leo tarehe 01 Oktoba ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala (DAS).

Uongozi wa BAGAMOYO KWANZA BLOG unamtakia kazi njema kwenye majukumu yake mapya ya uongozi.

No comments:

Post a Comment