Meneja Masoko na Mawasiliano wa GSM GROUP,
Matina Nkurlu,akikabidhi mabati kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Kaole, Ally Hiza, shule hiyo ipo kata ya Dunda Halmashauri ya Bagamoyo, mkoani Pwani.
.....................................
Kampuni
ya GSM GROUP imekabidhi msaada wa mabati 140 kwa Shule ya Msingi Kaole, wilayani Bagamoyo
ikiwa ni sehemu ya mchango wa Kampuni
hiyo katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kuhusu kuimarisha
miundombinu ya elimu hapa nchini.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi mabati hayo, Meneja Masoko na Mawasiliano wa GSM GROUP,
Matina Nkurlu, amesema msaada huo wameutoa ikiwa ni tabia waliyojiwekea
kushirikiana na wananchi na serikali kwa ujumla ili kutatua changamoto
zinazoikabili jamii.
Alisema
GSM GROUP imekuwa ikifanya hivyo mara kadhaa sehemu mbalimbali hapa nchini, lengo likiwa ni kuimarisha
uhusiano baina ya Kampuni hiyo na jamii sambamba na kuunga mkono juhudi za
serikali katika kuleta maendeleo.
Akizungumzia
msaada huo wa mabati shule ya Msingi Kaole, Matina alisema mara walipopata
barua ya maombi na kujiridhisha uhitaji wa mabati hayo haraka wakafanya
mchakato wa kufanikisha hilo, na hatimae wameweza kukabidhi msaada huo.
"
Tulipokea Barua ya maombi kupitia mlezi wenu wa shule na tukajiridhisha kuhusu
uhitaji huo na leo tumefanikiwa kuja kukabidhi mabati haya" Alisema
Matina.
Aidha,
alisema kuwa, kufuatia hali nzuri ya kiwango cha ufaulu na changamoto
zilizoainishwa kwenye ripoti ya shule hiyo, aliahidi kwamba watakaa tena kama ofisi
kuona ni kitu gani kingine wanaweza kusuaidia katika shule hiyo ili watoto
wapate elimu bora.
Aliongeza
kwa kusema kuwa, Serikali imejitahidi kuwezesha watoto kupata elimu bure nchi
nzima hivyo ni kazi ya wadau mbalimbali kuiunga mkono serikali na kusaidia
mapungufu yaliyopo katika shule.
Alisema
kujitolea kwa GSM GROUP kusiwe mwisho, na kutoa wito kwa makampuni na wadau kujitokeza kusaidia vitu mbalimbali katika shule hiyo.
Nae
Mlezi wa shule hiyo, Fimbo Butala, amesema anaishukuru Kampuni ya GSM GROUP kwa
msaada huo ambao umeweza kupunguza changamoto zilizopo shuleni hapo.
Butala
ameipongeza Kampuni ya GSM GROUP kwa usikivu wake wa kusikiliza kilio cha shule
hiyo ambapo ni muda mfupi baada ya kupokea barua ya maombi wakatekeleza ahadi
yao.
"Naomba
utufikishie salamu zetu kwa viongozi wa juu wa GSM GROUP kwamba tumefarijika
sana na ukarimu wenu kwa kutupatia msaada huu wa mabati ndani ya muda mfupi,
Mungu awabariki sana" Alisema Butala.
Awali
akitoa tarifa fupi ya shule hiyo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kaole, Ally
Hiza, alisema shule hiyo licha ya kuwa na ufaulu mzuri bado wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali, ikiwemo uchakavu wa majengo, ukosefu wa chumba cha
Maabara, pamoja na upungufu wa matundu ya vyoo.
Alitoa
wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza na kusaidia kile watakachoweza ili waweze
kuwa katika mazingira mazuri yatakayosaidia kuboresha kiwango cha taaluma
shuleni hapo.
Wanafunzi
wa shule hiyo, wamesema wanashukur kwa msaada huo wa mabati kwani paa la
madarasa bati zake zimetoboka hali inayopelekea kuvujiwa wakati wa mvua na
kushindwa kuendelea na masomo.
Walisema
mvua inaponyesha madarasa yanavuja kutokana na uchakavu wa mabati na
kusababisha madaftari na vitabu kuloa hali inayotia unyonge katika masomo.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa GSM GROUP,
Matina Nkurlu, (kulia) akisaidiana na walimu, wanafunzi na kamati ya shule kuteremsha mabati kutoka ndani ya Gari waliyobebea.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa GSM GROUP, Matina Nkurlu, (kushoto) akishuhudia mabati yakishushwa kutoka kwenye Gari walipowasili Shule ya Msingi Kaole wilayani Bagamoyo, katikati ni Mlezi wa shule hiyo, Fimbo Butala na kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Ally Hiza.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa GSM GROUP, Matina Nkurlu, (kushoto) akishuhudia mabati yakishushwa kutoka kwenye Gari walipowasili Shule ya Msingi Kaole wilayani Bagamoyo, katikati ni Mlezi wa shule hiyo, Fimbo Butala na kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Ally Hiza.
Muonekano wa jengo la Madarasa katika Shule ya Msingi Kaole wilayani Bagamoyo, ambalo bati zake zimetoboka na kusababisha kuvuja pindi mvua inaponyesha.
Na huu ni Muonekano wa paa la jengo la madarasa kama linavyoonekana kwa ndani ambapo bati zake zimetoka na kusababisha kuvuja pindi mvua inaponyesha.
No comments:
Post a Comment