Naibu waziri wa elimu sayansi na teknolojia wa kati kati akipiga makofi katika
halfa ya uwekaji wa jiwe la msingi katika ofisi ya kijiji cha kigoda
kilichopo kata ya Gwata katika halmashauri ya Kibaha vijini kushoto kwake ni
Mbunge wa Kibaha Vijijini Haoumd Jumaa, na viongozi wengine wa kijiji hicho.
Naibu
waziri wa elimu William Ole Nasha kushoto akiwa katika hafla ya uwekaji wa jiwe
la msingi pamoja na kutembelea eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya mradi wa
ujenzi wa shule mpya ya kata ya Gwata, kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha
vijijini Haoumd Jumaa.
(PICHA NA VICTOR MASANGU)
............................................
NA VICTOR MASANGU, PWANI
Naibu
Waziri wa elimu sayansi na teknolojia Williamu Ole Nasha amechukizwa
kuona vitendo vya baaadhi ya wazazi wa jamii ya wafugaji kutothamini suala la
elimu na kuamua kuwaozesha watoto wao mapema na kuwatumikisha katika kazi za
kuchunga mifugo.
Pia
amekemea na kulaani vikali vitendo hivyo na kuwataka kuhakikisha
wanawapeleka watoto wao shule ili kuunga mkono juhudi za serikali ya
awamu ya tano katika sekta ya elimu ikiwemo utoaji wa elimu bure.
Ole Nasha
ametoa kauli hiyo wakati wa halfa ya uwekaji wa jiwe la msingi katika
mradi wa ujenzi wa ofisi ya serikalI ya kijiji cha Kigoda kilichopo katika kata
ya Gwata Wilaya ya Kibaha sambamba na kutembelea eneo maalumu
ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari
ya kata ambayo itaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa wanafunzi ambao
wamekuwa wakitembea umbari wa kilometa nane kwenda kutafuta huduma ya elimu
katika maeneo mengine.
Aliongeza
kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuboresha sekta ya elimu
katika ngazi zote hivyo kitu kikubwa ni kuhakikisha watoto wanapatiwa malezi
bora ikiwemo kuwapeleka shule lengo ikiwa ni kuwapatia ujuzi na maarifa ambayo
yataweza kuliletea taifa maendeleo.
No comments:
Post a Comment