Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akimkabidhi Naibu Kamishna wa TAKUKURU Brigedia Jenerali
john Mbungo ripoti aliyokabidhiwa na kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa wakati
wa hotubia yake kwenye sherehe za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya
Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
zilizofanyika katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi. Oktoba 14,
2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akihotubia kwenye sherehe za Kilele za
Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba
wa Taifa Mwalimu Nyerere katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi. Oktoba
14, 2019.
..........................................
..........................................
Na
Hadija Hassan, Lindi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amkabidhi mkurugenzi wa
TAKUKURU Nchini Brigedia General John Mbugo, Ripoti ya miradi 107 yenye thamani
ya Shilingi bilioni 90.2 ambayo ilibainika kuwa na kasoro mbalimbali na
kukataliwa kuzinduliwa, kuonwa pamoja na kuwekwa mawe ya msingi na mbio za
Mwenge wa Uhuru 2019.
Magufuli
amekabidhi Ripoti hiyo mapema leo Oktoba14/2019 alipokuwa akiwahutubia wananchi
katika hafla ya maadhimisho ya kilele cha mwenge wa Uhuru, kumbukizi ya miaka
20 ya baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambalage Nyerere na wiki ya Vijana kitaifa
iliyofanyika katika Viwanja vya Ilulu Manispaa ya Lindi, Mkoani Lindi.
Rais
Magufuli alimtaka Mkuu huyo wa TAKUKURU Nchini kufanya ufuatiliaji kwa kina wa
taarifa hizo za miradi ikiwa ni pamoja na kumpelekea mapendekezo na namna
atakavyoshughulika na watu ambao miradi yao ilibainika kuwa chini ya kiwango.
“Nakukabidhi
hii ripoti ya miradi ambayo imeonekana imekuwa na dosari ambapo mbio hizi za
mwenge wa Uhuru zimekataa kuzindua, kukagua pamoja na kuiwekea mawe ya msingi,
kwako ukafanye uchambuzi wa kila ukurasa, kila nukta, ukachambue na wale wote
watakao husika usisite kuwapeleka mahakamani na wale wengine utakaowaona
wakubwa wakubwa unafikiri ni vigumu niletee ripoti yao nitashugulikanao mimi
mwenyewe” Alieleza Dkt Magufuli “
"Lengo
la kufanya hivi tunataka Tanzania inyooke hatuwezi tukawa tunapeleka fedha halafu
wengine wanachezea tuu na ndio maana nawapongeza vijana hawa wakimbiza mwenge
wa Uhuru, hawa ndio Taifa la kesho ni lazima tujenge Taifa lao, tuwaandalie
mazingira ya kutawala vizuri” alisisitiza Dkt, Magufuli.
"Mara
zote mbio za mwenge wa Uhuru pamoja na mambo mengine unatumika katika kufanya
Tathmini ya ubora wa miradi mbali mbali ya Maendeleo pamoja na matumizi ya
fedha za Umma kwenye miradi hiyo na hiyo kazi imefanyika vizuri, tumepewa
taarifa ya miradi yenye dosari mbali mbali ikiwemo yenye viashiria vya ubadhilifu
wa fedha na ni matumaini yangu kwamba ofisi ya Waziri Mkuu pia itafuatilia
miradi hii” aliongeza Dkt Mgufuli.
Awali
waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu sera , vijana na Watu wenye ulemavu Jenista
Muhagama alisema miradi 107 yenye thamani ya Shilingi bilioni 90.2 katika
halmashauri za wilaya 82 ilitiliwa mashaka na hatimae kushindwa kuzinduliwa ama
kutowekewa mawe ya msingi.
Mhagama
alizitaja baadhi ya kasoro zilizoainishwa na mbio za mwenge wa Uhuru ni pamoja
na eneo la Matumizi ya fedha nyingi yasiyoendana na thamani halisi ya Mradi
husika, Miradi kujengwa kinyume na mikataba ya ujenzi na makadilio
yaliyopitishwa na wataalamu (BOQ), wakandarasi kushindwa kufuata na kusimamia
kanuni za ujenzi zilizoainishwa kwenye BOQ katika baadhi ya Miradi inayojengwa
na hivyo kufanya Ubora wa miradi hiyo kutia shaka hasa katika swala la uimara
na uwendelevu wa miradi hiyo.
Alizitaja
kasoro zingine kuwa ni matumizi ya vifaa duni vya ujenzi katika miradi ya Umma
iliyogharimu Fedha nyingi, wahandisi katika baadhi ya halmashauri kutowasimamia
vizuri wakandarasi jambo linalotia shaka juu ya utekelezaji wa majukumu ya
watumishi hao, Wakandarasi kutomaliza miradi wanayopewa kwa wakati na mamlaka
husika kutokuwachukulia hatua za kisheria na kuacha miradi inaendelea kuzagaa
bila kukamilika kwa muda mrefu.
Kasoro
zingine ni ubora wa miradi usioridhisha kabisa katika baadhi ya miradi ya maji
hasa ujenzi wa visima vya juu vya kuhifadhia Maji ambavyo kuta zake zimetapakaa
nyufa na kuchakaa kabla ya miradi hiyo kuanza kutumika, udanganyifu unaojificha
katika lugha za kitaalam hasa katika miradi ya Maji na Miradi ya Ujenzi.
Hali
hiyo inakuwa vigumu kwa viongozi ambao hawana utaalamu kubaini matumizi ya
Fedha za Umma zilizotumika vibaya kwa kichaka hicho, vitendo visivyo vya
kizalendo vya kufanya makadilio ya ujenzi wa miradi (BOQ) zisizoendana na
gharama zilizosokoni zinazofanywa na baadhi ya wahandisi wa Halmashauri katika
miradi inayotekelezwa chini ya utaratibu wa “FORCE ACOUNT”.
Hata
hivyo Muhagama alizitaja Halmashauri hizo 80 ambazo zilikutwa na miradi yenye
kasoro kuwa ni pamojana na mbozi DC, Songwe DC, Ileje DC, Tunduma TC,
Sumbawanga DC, Sumbawanga MC, Karagwe DC, Msimbo DC, Mpanda MC, Uvinza DC,
Kigoma MC, Buhingwe DC, Kasulu DC, Kibondo DC, Ngala DC, Bukoba MC, Bialamulo
DC, na Bukombe DC.
Zingine
ni Geita DC, Geita TC, Nyamwale DC, Msalala DC, Kahama TC, Misungwi DC,
Sengerema DC, Buchofya DC, Ilemela MC, Kwimba DC, Meatu DC, Itilima DC, Buliadi
TC, Bunda DC, Musoma DC, Lorya DC, Talime TC, Talime DC, Longido DC, Mmemo DC,
Babati DC, Kiteto DC, Rombo DC, Mwanga DC, Bumbuli DC, Kilindi DC, Handeni DC,
Korongwe TC, Muheza DC, Pangani DC, Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja , Wilaya ya
kati Unguja, kusini “A” Mjini maghalibi.
Ubungo
MC, Temeke MC, Kibiti DC, Rufiji DC, Mafya DC, Kibaha DC, Mvomelo DC, Malimi
DC, Ifakala TC, Gailoba DC, Mwapwa DC, Kondoa TC, Dodoma CC,
Itingi DC, Mkalama DC, Ilamba DC,Igunga DC, Nzega DC, Tabora MC, Chunya MC,
Busokelo MC, Kyela DC, Rungwe DC, Iringa DC, Mbaleli DC, Mufindi DC, Iringa MC,
Wangig’ombe DC, Njombe DC, Malamba DC, Songea DC, na Nyasa DC
Akisoma
risala ya utii kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mbele ya
Rais Magufuli alisema kuwa mwenge huo wa uhuru mwaka 2019 umekimbizwa kwa
umbali wa km 26, 273.94 katika mikoa 31, halmashauri za wilaya 195 kwa
siku 195 na kutembelea, kukagua, kufungua na kuzindua miradi ya maendeleo 1,390
Kiongozi
huyo wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa Mkongea ally akiwasilisha risara
ya utii alimueleza Rais, Magufuli kuwa kazi ya kupambana na ubadhirifu
katika baadhi ya miradi ya maendeleo kwao haikuwa rahisi kutokana na
vikwazo mbali mbali kama vile vitisho pamoja na kejeli zenye lengo la
kuwakatisha tamaa zilifanywa na baadhi ya viongozi hao.
Hata
hivyo Mkongea aliwaasa viongozi pamoja na wananchi kuendelea kudumisha
ushirikiano waliokuwa wanauonyesha wakati mbio za mwenge zilipokuwa zimefika
katika maeneo yao kwa kuwa pamoja na mambo mengine dhamira ya mwengi ni
kudumisha upendo na mshikamano
Pamoja
na mambo mengine Mkongea alimuomba Rais magufuli Kuongeza uwekezaji na
ufuatiliaji wa karibu katika miradi ya maji na kuchukuwa hatua stahiki
kwa wale wote wanaobainika kuhujumu, sekta hiyo muhimu kwa ustawi
wa kitaifa.
No comments:
Post a Comment