Na
Hadija Hassan, Lindi.
Halmashauri
zimetakiwa kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu (walemavu) ambao wamepewa
mikopo ya asilimia 2 inayotokana na asilimia 10 ya fedha za mapato ya Ndani
katika Halmashauri zao kuwatafutia masoko ya uhakika ya bidhaa wanazozizalisha
ili kuhakikisha fedha walizokopa wanarejesha kwa wakati.
Wito
huo Umetolewa na kiongozi Wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Mzee Mkongea Ally alipotembelea na kuona kazi mbali mbali za
mikono zinazofanywa na vikundi vya wajasiriamali wa Halmashauri ya wilaya ya
Lindi ambavyo vimepewa mikopo ya asilimia 10 kutoka Halmashauri.
Ally,
alisema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo kundi, hilo ni kushindwa
kutangaza bidhaa walizozizalisha ukilinganisha na makundi mengine kama ya
vijana na Wanawake jambo ambalo huwafanya kushindwa kurejesha mikopo hiyo kwa
wakati.
Alisema
Serikali ilivyoamua kutoa mikopo hii ilikuwa na lengo la kuwawezesha wananchi
kiuchumi pamoja na kuwawezesha kuondokana na umasikini hivyo ni wajibu wa
Halmashauri kusaidia kundi hilo muhimu.
Awali
afisa maendeleo ya jamii wa Halmashauri hiyo ya Lindi Grace Mwambe alisema kuwa
Halmashauri hiyo ipo msitari wa mbele katika kuwawezesha Wananchi kiuchumi hasa
kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
Alisema
katika kutekeleza maagizo ya Serikali juu ya kukopesha makundi hayo kwa
asilimia 10 za fedha zinazopatikana katika mapato ya ndani.
Halmashauri
hiyo imeweza kutoa kiasi cha shilingi milioni 27 kwa mwaka wa fedha wa
2019/2020 kwa vikundi 17.
Aidha
akiongeza kuwa kati ya vikundi hivyo 17 vilivyopewa mikopo hiyo , vikundi 7 vya
vijana, vikundi 8 vya wanawake na 1 cha watu wenye ulemavu
No comments:
Post a Comment