Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Ha Harrison
Mwakyembe, akizungumza wakati wakufungua rasmi Tamasha la 38 la Kimataifa la Sanaa na
Utamaduni, Ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)
mjini Bagamoyo.
.....................................
.....................................
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Ha Harrison
Mwakyembe ametaka kiswahili kitumike katika kufundisha sanaa hasa zile zenye
maudhui ya kiswahili ili kukuza lugha hiyo ndani na nje ya Tanzania.
Dkt.
mwakyembe ameyasema hayo leo Oktoba 19, 2019 kwenye uzinduzi wa Tamasha la 38 la Kimataifa la Sanaa na
Utamaduni uliofanyika Ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)
mjini Bagamoyo.
Alisema
chuo hicho cha sanaa ambacho ni kikongwe hapa nchini kwa kutoa elimu ya sanaa
za aina mbalimbali, ni vyema sasa kikatumia kiswahili katika ufundishaji wake.
Aliendelea
kusema kuwa, mataifa mbalimbali hufika chuoni hapo kujifunza sanaa hivyo
wanapofundishwa kwa lugha ya kiswahili itakuwa rahisi nao kuitangaza lugha hiyo
kwenye nchi zao.
Alisema
katika kukuza utamaduni wa mtanzania kiswahili na sanaa ni vitu vinavyoenda
pamoja na kamwe haviwezi kutenganishwa.
Dkt.
Mwakyembe ameupongeza uongozi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, (TaSUBa)
kwa kufanikiwa kuandaa Tamasha hilo ambalo limejumuisha watu kutoka nchi
mbalimbali.
Alisema
kitendo cha kuandaa Tamasha hilo kisha kuhudhuriwa na watu kutoka mataifa
mbalimbali huku mkiungwa mkono na wadhamni wa mbalimbali katika kufanikisha ni
ishara kuwa chuo hicho kina kubalika kwa wakazi wa Bagamoyo, watanzania wote na
nchi mbaalimbaali duniani.
Aliongeza
kwa kusema kuwa, matamasha kama hayo ni muhimu katika kukuza Uchumi wa nchi,
Utalii, mahusinaao mema baina ya Tanzania na nchi marafiki kwa kuwaalika na
kuhudhuria kwao.
Alitumia
nafasi hiyo kuwataka wakazi wa Bagamoyo kuhudhuria katika tamasha hilo katika
siku zote za maonyesho ili waweze
kujionea mambo mbalimbali yanayofundishwa katika chuo hicho yakionyeshwa kwa
vitendo.
Kwa
upande wake Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)
Dkt. Herbert Makoye amesema amesema anawashukuru wale wote walioshiriki katika
kufanikisha Tamasha hilo.
Alisema lengo kuu la Tamasha hilo ni kuendeleza na Kudumisha utamaduni wa Mtanzania, kubadilishana uzoefu na kujifunza kutoka kwa mataifa mengine kupitia warsha, kongamano na maonyesho mbalimbali.
Aidha, aliongeza kuwa pia Tamasha hilo linatoa fursa kwa wasanii, wa ndani na nje ya nchi pamoja na watanzania kwa ujumla kukutana na kuenzi utajiri wa utamaduni wao unaowatoafutisha na mataifa mengine.
Alisema lengo kuu la Tamasha hilo ni kuendeleza na Kudumisha utamaduni wa Mtanzania, kubadilishana uzoefu na kujifunza kutoka kwa mataifa mengine kupitia warsha, kongamano na maonyesho mbalimbali.
Aidha, aliongeza kuwa pia Tamasha hilo linatoa fursa kwa wasanii, wa ndani na nje ya nchi pamoja na watanzania kwa ujumla kukutana na kuenzi utajiri wa utamaduni wao unaowatoafutisha na mataifa mengine.
Nae
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa, amewataka washiriki wa
tamasha hilo kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo katika wilaya hiyo ili
waweze kujionea mambo mbalimbali ikiwemo historia pamoja wanyama wanaopatikana
katika mbuga yaa Saadani.
Alisema
Bagamoyo ni mji mkongwe ambao watu wake ni wakarimu hivyo wageni waliofika
katika tamasha hilo wanaweza kutembea hali ya kuwa huru katika maeneo
mbalimbali ya Bagamoyo.
Akizungumza
kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Afisa Tawala wa wilaya ya
Bagamoyo, (AO) Zubeda Omari amesema
Kamati ya Ulinzi na Usalama imeimarisha ulinzi katika kipindi chote cha tamasha
na kwamba wageni wasiwe na hofu ya aina yoyote.
Tamasha
la kimataifa la sanaa na utamaduni hufanyika kila mwaka ambapo mwaka huu ni la
38 ambalo limebeba kauli mbiu isemayo "Sanaa na Utamaduni Ajira yangu"
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Ha Harrison
Mwakyembe (katikati) akiangalia kazi mbalimbali zilizofanywa na wasanii katika mabanda yaliyopo viwanja vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) mjini Bagamoyo leo Oktoba 19, 2019, kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Ally Possi, na kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)
Dkt. Herbert Makoye.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye, akizungumza katika ufunguzi wa Tamasha la 38 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni uliofanyika Ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) mjini Bagamoyo, leo Oktoba 19, 2019.
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 38 la Kimataifa la Sanaa na
Utamaduni uliofanyika Ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)
mjini Bagamoyo, leo Oktoba 19, 2019.
Afisa Tawala wa wilaya ya
Bagamoyo, (AO) Zubeda Omari, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo, kwenye ufunguzi wa Tamasha la 38 la Kimataifa la Sanaa na
Utamaduni uliofanyika Ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)
mjini Bagamoyo, leo Oktoba 19, 2019.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Ha Harrison Mwakyembe, akipiga ngoma kuashiria kufunguliwa kwa Tamasha la 38 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni katika Ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) mjini Bagamoyo, leo Oktoba 19, 2019.