NA
HADIJA HASSAN, LINDI
TAASISI
ya kuzuia na kupambana na Rushwa (YAKUKURU) Mkoa wa Lindi ImeendeLea kuwakamata
viongozi wa vyama vya Msingi (AMCOS) 99 kutoka 51, Wa awali ambao wamehusika
katika kudhulumu fedha za Wakulima wa Ufuta wa Mkoa huo.
Ukamatwaji
wa viongozi hao ni moja ya utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli
alilolitoa oktoba 10 mwaka huu wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa
Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi, ambapo aliiagiza TAKUKURU pamoja na Naibu
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kuhakikisha vyama 10 vya Msingi (AMCOS)
vinavyodaiwa na wakulima wa ufuta vinawalipa wakulima hao fedha zao kabla ya
msimu mpya wa Korosho kuanza.
Akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Brigedia General John Mbungo alisema kuwa ongezeko
la viongozi hao wa Vyama vya msingi limekuja baada ya taasisi yao kuendelea
kufanya msako katika baadhi ya vyama vya Msingi (AMCOS) Mkoani humo
"ingawa
Taarifa iliyokabidhiwa TAKUKURU na Naibu Waziri wa kilimo Mhe, Hussein Bashe
ilikuwa inaonyesha wakulima wa ufuta wamedhulumiwa kiasi cha shilingi milioni
436,869, 982,00 na vyama 10 vya msingi (AMCOS) lakini uchunguzi na ufuatiliaji
uliofanywa na TAKUKURU ulibaini kuwepo kwa vyama 31 vya Msingi (AMCOS) Kuwadhulumu
wakulima wa ufuta kiasi cha shilingi Bilioni 1,236,363,075.00/=" alisema
Mbungo.
Hata
hivyo Mbungo alisema kuwa tokea zoezi hilo la kuwakamata viongozi wa vyama vya
msingi (AMCOS) oktoba 16, mpaka oktoba 19 tayari kiasi cha shilingi milioni
255,598,194.00 zimerejeshwa katika Ofisi ya TAKUKURU na kwamba fedha hizo
zitaanza kulipwa kwa wakulima hao kwa utaratibu utakaopangwa.
Mbungo
pia alisema katika kuhakikisha wakulima wote waliodhulumiwa fedha zao wanapata
haki zao Taasisi hiyo imeanza zoezi la kutambua, kupiga picha na kukamata Mali
za viongozi hao wa AMCOS wanaodaiwa ili ziwe dhamana ya madeni wanayodaiwa na
endapo watashindwa kulipa kwa muda waliokubaliana vitu hivyo vitauzwa ili
kulipa madeni ya wakulima.
Aidha,
alitoa rai kwa viongozi wote wa vyama vya ushirika Nchini vinavyodaiwa na wakulima
walipe wakulima hao haraka iwezekanavyo kabla ya TAKUKURU haijawafikia kwani
zoezi hilo litakuwa endelevu na kwamba hakutakuwa na chama chochote cha
ushirika kinacho daiwa kitakachobaki salama
No comments:
Post a Comment