Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Bi Kasilda Mgeni, akipata maelezo kuhusu hali ya uandikishaji wapiga kura katika jimbo la Chalinze.
.......................................
Na
Shushu Joel
Katibu
tawala wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Bi Kasilda Mgeni, amefurahishwa na
wananchi wa halmashauri ya chalinze kwa kuweza kuitikia wito wa kujiandikisha
kwenye daftali la kupiga kura.
Wananchi
wamekuwa mstari wa mbele katika zoezi la kujiandikisha kutokana na uelewa wa
kutumia fursa ya kuwachagua viongozi wao.
Akizungumza
na baadhi ya wananchi katika moja ya vituo vya kujiandikishia alivyotembelea
kwenye kata ya ubena, halmashauri ya chalinze katibu tawala huyo aliwapongeza
wananchi waliojiandikisha na kuwataka wawahamasishe na wenzao ambao bado ili
nao wajiandikishe kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji
unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi na moja.
"Kwa
kweli chalinze wananchi hongereni sana kwa kujiandikisha kwa wingi nadhani
kufikia mwisho wa zoezi hili mtakuwa mmevuka lengo lenu" Alisèma.
Aidha
Mgeni amempongeza mbunge wa jimbo la chalinze mh. Ridhiwani Kikwete kwa kazi
kubwa anayoifanya ya kuhamasisha wananchi wake ili wakajiandikishe.
Aliongeza
kuwa Kikwete ni kiongozi wa pekee aliyefanikisha kazi ya hamasa kwa wananchi
kwani watu wamejitokeza na wanazidi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya
kujiandikisha na kwa baadhi ya vituo kuonekana wamemaliza kuandikisha huku
wakiwa wamevuka malengo yaliyokuwa yamekusudiwa.
Kwa
upande wake mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete alisema kuwa ujio wa kamati
ya ulinzi na usalama ikiongozwa na katibu tawala imemuongezea nguvu na mzuka
zaidi.
Alisema
kuwa wananchi wa chalinze wamehamasika wenyewe mara baada ya kutangaziwa na
gari maalum lililotolewa na halmashauri kwa ajili ya kuwahamasisha wakazi wa
chalinze kuweza kujitokeza.
Aidha
Aliongeza kuwa kila kazi inachangamoto zake lakini kwa chalinze changamoto
kubwa ni mfululizo wa mvua zilizokuwa zikinyesha hivyo kupelekea wananchi
kutojitokeza huku wengine wakiwa mashambani.
"Kwa
jinsi hali inavyoelekea wanachalinze tutavuka malengo tuliyokuwa tumejiwekea
kwani kwa sasa tuna zaidi 80% huku siku chache zikiwa zimebaki.
Naye
msimamizi mkuu wa uchaguzi katika halmashauri hiyo Shabani Milao amempongeza
mbunge kwa jinsi alivyojitolea kutoa hamasa kwa wananchi katika zoezi zima la
kujiandikisha.
Aliongeza
kuwa zoezi linaenda vizuri na wanataraji kufikia lengo lililokusudiwa. kilichokuwa
kimekusudiwa na serikali.
Katibu tawala wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Kasilda Mgeni, akipata maelezo kuhusu hali ya uandikishaji wapiga kura katika jimbo la Chalinze, pembeni yake ni Mbunge wa hilo, Ridhiwani Kikwete na kulia msimamizi wa uchaguzi katika halmashauri hiyo Shabani Milao.
Katibu tawala wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Kasilda Mgeni, akiwa amefuatana na msimamizi wa uchaguzi katika halmashauri ya Chalinze Shabani Milao, wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama (KUU) wilaya, ilipotembelea halmashauri hiyo kukagua vituo vya uandikishaji wapiga kura.
Picha
chini na juu zikimuonyesha Katibu Tawala wilaya ya Bagamoyo, Bi Kasilda Mgeni
akifuatana na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwet na Msimamizi wa Uchaguzi
Halmashauri ya Chalinze, Shabani Milao, wakati Kamati Kamati ya Ulinzi na
Usalama wilaya ilipofanya ziara katika halmashauri hiyo kukagua vituo vya
uandikishaji wapiga kura.
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwet, akizungumza katika moja ya vituo vya kuandikisha wapiga kura wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Bagamoyo, ilipotembelea katika jimbo hilo ikiongozwa na Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Bi Kasilda Mgeni.
No comments:
Post a Comment