Na
Alodia Dominick, Bukoba.
Mahakama
kuu Kanda ya Bukoba Mkoani Kagera imeendelea kusikiliza ushahidi wa upande wa
mdaiwa katika kesi ya madai namba 12 ya mwaka 2016 ya shilingi 1 bilioni moja na
milioni 216 fidia ya udhalilishaji iliyofunguliwa na mbunge wa Bukoba Vijijini
Jasson Rweikiza dhidi ya mdaiwa Novatus Rwechungura Nkwama mjumbe wa
halmashauri kuu ya Chama cha mapinduzi ( CCM ) Mkoa wa Kagera.
Shahidi
wa mtuhumiwa Raurent Buteni (59) akitoa ushahidi wake mahakamani akiongozwa na
wakili Dastan Mujaki ameeleza mahakama kuu mbele ya Jaji Dk. Ntemi
Kilekamajenga wa mahakama hiyo kuwa julai tano mwaka 2016 ulikuwepo mkutano wa
kitongoji cha Buryankuro na yeye alikuwa katibu wa mkutano huo ambao ulikuwa na
ajenda tatu ambazo ni kufungua, kujadili wizi wa ndizi na ndizi kali uliokuwa
katika kitongoji hicho na ajenda ya kufunga.
Baada
ya wakiri Dastan Mujack kumuhoji shahidi juu ya kashifa zinazotajwa dhidi ya
mshitakiwa kuwa alimkashifu Jasson Rweikiza kuwa ni mwizi na alishirikiana na
Novatus Nkwama kuchakachua kura za mwaka 2015 wakati amepata ubunge, Shahidi
Buteni ameeleza mahakama kuwa, hakuna maneno ya kashfa yaliyoongelewa kwenye
mkutano huo kwani yangeongelewa muhusika angetolewa katika mkutano huo.
Naye
wakili wa upande wa Mdai Alli Chamani akimuhoji shahidi wa upande wa mdaiwa
amemuuliza kwamba, katika eneo la mkutano waliweka bango la kuonyesha kuwa ni
mkutano wa kitongoji? na katika eneo la mkutano ilikuwepo barabara iliyokuwa
inakatiza? na je mwanakitongoji jirani alikuwa anaruhusiwa kuhudhuria mkutano
huo?.
Akijibu
maswali hayo, shahidi Buteni amesema kuwa, katika eneo la mkutano liliwekwa
bango la kuonyesha kuna mkutano na hivyo hakuna mwananchi wa kitongoji jirani
aliyeruhusiwa kuhudhuria mkutano huo na ilikuwepo barabara inayokatisha kutoka
kitwe kwenda Amugenge.
Aidha
katika kesi hiyo upande wa mdai ambaye ni Mbunge Jasson Rweikiza mashahidi
wanane tayari wametoa ushahidi wao na upande wa mdaiwa Novatus Nkwama mashahidi
watatu tayari wametoa ushahidi wao mahakamani na bado shahidi mmoja ambaye
atatoa ushahidi wake octoba 18 mwaka huu kesi itakapotajwa tena
No comments:
Post a Comment