Kiongozi
wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa Mzee Mkongea Ally,(katikati) akizungumza na wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa kituo cha Radio cha Mashujaa fm. wilayani Nachingwea jana Oktoba 10, 2019, kulia ni Mkuu wa wilaya ya hiyo, Rukia Muango, na kushoto ni Meneja wa Mashujaa fm, Zakia Gaspa.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa Mzee Mkongea Ally, akifungua kitambaa kwenye jiwe la msingi ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi ujenzi wa kituo cha Radio cha Mashujaa fm. wilayani Nachingwea jana Oktoba 10, 2019, anaeonekana kwa mbele akiwa na furaha ni Meneja wa Mashujaa fm, Zakia Gaspa.
PICHA ZOTE NA HADIJA HASSAN.
..........................................
Na
Hadija Hassan, Lindi.
Kiongozi
wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa Mzee Mkongea Ally, amewataka wanahabari Nchini
kuandika habari kwa Kuzingatia weledi pamoja na maadali ya habari.
Mkongea
ametoa wito huo jana Oktoba 10, 2019 wakati wa kuzindua mradi wa ujenzi wa
kituo cha Radio ya Mashujaa Fm, wilayani Nachingwea Mkoani Lindi uliofanywa na
mbio hizo za mwenge.
Alisema
vyombo vya Habari na wanahabari kwa jumla wamekuwa na nafasi kubwa katika jamii
kwa masuala ya kuelimisha, kuburudisha na hata kuhabarisha hivyo ni vyema kwa
wanahabari kuhakikisha habari wanazozitoa ziwa ni zenye uhakika na zisizokuwa
na uchochezi.
"Hii
ni kwa sababu ulimi wa mwanahabari ukikosea kidogo urekebishaji wake unakuwa na
kazi kubwa, hivyo hakikisheni mnafanya kazi kwa uangalifu ili kile ambacho
kinafanyika ndicho kinachomfikia mwananchi au mwanajamii" alisisitiza
Mkongea.
Awali
Meneja wa mashujaa FM, Zakia Gaspa akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi wa kituo
hicho cha Radio alisema kuwa kituo hicho hadi kukamilika kwake kimeghalimu
kiasi cha shilingi milioni 15 Gaspa alisema katika kuhakikisha inasaidiana na
Serikali katika mambo mbalimbali ya maendeleo radio yao imekuwa Ikijikita
katika shughuli mbali mbali za kijamii ili kuhakikisha wananchi wanashiriki
katika shughuli za kimaendeleo.
No comments:
Post a Comment