Tuesday, October 1, 2019

AFISA TARAFA WA MSATA BAGAMOYO ATEULIWA KUWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA UYUI TABORA.

Image may contain: 1 person, closeup
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, leo Tarehe 01 Oktoba 2019 amefanya uteuzi na kuwahamisha vituo vya kazi Wakurugenzi wa Halmashauri za Manispaa na Wilaya, na pia amefanya uteuzi wa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocol).


Katika uteuzi huo aliyekuwa Afisa tarafa wa Msata iliyopo Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo, Said Hemed Magaro, ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora.


BAGAMOYO KWANZA BLOG inatoa salamu za pongezi kwake na tunamtakia kazi njema katika majukumu yake mapya ya uongzi.

No comments:

Post a Comment