Thursday, October 3, 2019

MBUNGE JUMAA ACHANGIA MADARASA MAWILI NA HEKARI KUMI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI GWATA

Mbungewa Jimbo la Kibaha vijijini Haoumd Jumaa akizungumza na baadhi ya wananchi wa  kata ya Gwata hawapo pichani wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi kwa ajaili ya ofisi ya kijiji cha kigoga pamoja na kujoinenea eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya kata.
 
Mbunge wa Jiambo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa kushoto akikabidhiwa zawadi ya fimbo  na mmoja wa viongozi wa jamii ya wafugaji alipowasili katika kijiji cha Kigoda, kulia kwake ni Naibu waziri wa elimu sayansi na teknolojia William Ole Nasha baada ya kuwasili katika eneo hilo  kwa lengo la kuweka jiwe la msingi katika ofisi ya kijiji hicho pamoja na kutembelea eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya kata 
 (PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
.................................

NA VICTOR  MASANGU, PWANI.
 
Mbgunge wa Jimbo la Kibaha vijijini Hamoud Jumaa katika kuunga juhudi za Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe ,Magufuli katika sekta ya elimu ameamua kutoa eneo la hekari kumi  pamoja na kuahidi ujenzi wa madarasa mawili kwa lengo la kuanzisha mradi wa ujenzi wa shule ya kata ya Gwata ambayo itapunguza kwa  kiasi kikubwa  adha  kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata shule.


Mbunge Jumaa ametoa ahadi hizo wakati akizungumza kwenye ziara ya Naibu Waziri wa Elimu Williamu Ole Nasha alipotembelea kijiji cha Kigoda kilichopo kata ya Gwata Wilaya ya Kibaha.


“Kwanza kabisa napenda kumpongeza Naibu waziri wa elimu kwa kuja kufanya ziara katika kijiji hiki na mimi napenda kumuahidi kuwa maelekezo yake yote ya kuongeza hekari zingine mimi nipo tayari kwa hiyo mimi ninataongeza hekari zingine tano kwa hiyo jumla zitakuwa kumi hii yote ni kuhakikisha tunaunga mkono juhudin za serikali ya awamu ya tano katika kuboresha elimu,”alisema Jumaa.


Aidha Jumaa katika hatua nyingine amesema lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba analeta mabadiliko chanya ya kimaendeleo katika Nyanja mbali mbali kwa kutimiza ilani ili wananchi wafaidike uongozi huu wa serikali ya awamu ya tano inayojali watu wa aina zote wakiwemo wanyonge.


Alisema atashirikiana bega kwa bega na wananchi pamoja  na serikali kwa ajili ya kukamilisha mradi wa ujenzi wa shule hiyo ya kata ya Gwata ambayo itakuwa ni msaada mkubwa katika kuwaondolewa wanafunzi changamoto ya kutembea umbali mrefu.


Pia aliwaasa wazazi na walezi wa jamii ya wafugaji kumuunga mkono Rais wa awamu ya tano Dkt. John  Pombe Magufuli katika kuhakikisha kwamba watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanapelekwa mara moja shule, ili kuwapatia haki yao ya msingi pamoja na kuwataka kuachana na tabia ya kuwakatisha masomo bila sababu zozote za msingi.


Kumekuwepo na wimbi la baadhi ya jamii ya wafugaji katika Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani kuamua kuwakatisha watoto wao masomo na kuwatumikisha katika kazi mbali mbali ikiwemo kuwapeleka maporini kwa ajili ya kuchunga Ng’ombe na mbuzi pamoja na wengine kuwaozesha kitu ambacho kinawanyima haki zao za msingi ikiwemo suala la elimu.


Akizungumza katika mkutano huo, Naibu Waziri wa elimu sayansi na teknolojia, Williamu Ole Nasha, alimpongeza Mbunge huyo kwa kuwasimamia wananchi katika swala la maendeleo.


“Nampongeza sana Mbunge wa jimnbo la Kibaha Vijijini kwani amekuwa ni mtu mwenye kunisumbua  sana lakini lengo lake kubwa ni kuwaletea maenedeleo wananchi wake, kwa hiyo kikubwa zaidi tumuunge mkono katika kuleta mabadiliko na hili tabia ya kuwaozesha watoto wenu kwa kweli mimi nataka muiache kabisa na kuwachungisha ng’ombe,”alisema Naibu wazri, Ole Nasha.


Mmoja wa  wazazi wa jamii ya wafugaji  akizungumza kwa niaba ya wenzake aliahidi kulitekeleza na kulivalia njuga agizo ambalo limetolewa na Naibu Waziri na kwamba wataweka mipango madhubuti ya kuwapatia watoto wao haki zao za msingi ikiwemo kuwapeleka shule pamoja na kuachana na tabia ya kuwatumiksiha kwa kipindi kirefu katika kuchunga

No comments:

Post a Comment