Wednesday, October 9, 2019

MWENGE WA UHURU KUKAGUA MIRADI YA BILIONI 12 LINDI.

Na Hadija Hassan, Lindi.

Mwenge wa uhuru umewasili Mkoani Lindi ukitokea Mkoani Mtwara ambapo jumla ya miradi ya Maendeleo 28 yenye Thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 12, inatarajiwa kupitiwa.

Mwenge huo wa uhuru umewasili jana Mkoani Lindi na kufanyika makabidhiano katika Kijiji cha Madangwa Halmashauri ya wilaya ya Lindi Mkoani humo na unatarajiwa kukimbizwa katika Halmashauri sita za Mkoa huo.

Akitoa taarifa ya mapokezi ya mbio za Mwenge wa Uhuru, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, baada ya makabiziano hayo, alisema kati ya miradi hiyo 28 miradi 9 itawekwa mawe ya msingi ,8 itazinduliwa, 8 itakaguliwa na 3 itafunguliwa.

Aidha Zambi alisema kuwa Mwenge huo wa uhuru unatarajiwa kukimbizwa Umbali wa Km.950.7 katika Wilaya za Lindi, Ruangwa, Nachingwea, Liwale, Kilwa na Mansipaa ya Lindi Mkoani humo.

Nae mkimbiza mwenge kitaifa Mzee Mkongea Ally aliwataka wataalamu wanaohusika na miradi kuwepo kwenye miradi yao wakati wote ambao mwenge utafika katika maeneo yao

No comments:

Post a Comment