Mkuu wa
mkoa wa Arusha akipata maelezo namna ga kujiandikisha kwenye daftari la kupiga
kura jana Oktoba 09, 2019, ambapo yeye ni mkazi wa eneo hilo.
Mkuu wa
mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akipata maelekezo namna ya kujiandikisha kwenye
daftari la wapiga kura katika kata ya Murieti ambapo yeye ni mkazi wa eneo
hilo.
....................................
Na Vero Ignatus,Arusha.
Zaidi ya wakazi milioni 1.9 mkoa wa Arusha
wanatarajia kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura la uchaguzi mdogo wa
serikali za mitaa ili kuweza kutimiza haki yao ya msingi ya kikatiba ya
kuchagua viongozi wanaowataka kwa ajili ya kujiletea maendeleo katika Nyanja
zote.
Richard Kwitega ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha
amesema kuwa wananchi hao watapiga kura watakuwa na sifa ya umri wa miaka 18 na
kuendelea huku wakiwa na sifa za kuwa wakazi wa eneo husika wanakojiandikishia
na kupiga kura .
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amefika na
kujiandikisha katika daftari la kupiga kura, katika kata ya Muriet ambako ni
mwenyeji wa eneo hilo, amesema kuwa serikali imeweka mazingira rafiki kwa watu
wote kujiandikisha bila kujali itikadi za vyama vyao wote wanapaswa kushiriki
katika zoezi hilo la kujiandikisha.
Msena Bina ni msimamizi wa Uchaguzi jiji la Arusha
amesema kuwa vituo vimefunguliwa 154 kwa ajili ya wananchi kujiandikisha hivyo
amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana
amesema kuwa jeshi hilo litaimarisha hali ya ulinzi na usalama, na kufanya kazi
bila kupendelea chama chochote, kama walivyotoa maelekezo kwa Askari kufanya
kazi kwa uadilifu na uzalendo.
No comments:
Post a Comment