Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza wakati alipokuwa akifungua kikao
kati ya wizara hiyo na wahariri wa vyombo vya habari uliofanyika katika taasisi
ya NACTE Mwenge jijini Dar es salaam.
..............................
Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo amewapongeza waandishi wa habari kwa kazi
kubwa wanayofanya ya kuhabarisha Wananchi kuhusu masuala ya sekta ya elimu na
Serikali kwa ujumla.
Dkt. Leonard Akwilapo ameyasema hayo
wakati wa kikao kati ya wahariri wa vyombo vya mbalimbali vya habari na wizara
hiyo ambapo alielezea kiwango cha elimu nchini na kusema kinaendelea
vizuri na hatua mbalimbali zinafanyika kuiboresha sekta ya elimu.
Ameongeza kuwa Dira ya wizara ni kuwa
na Mtanzania aliyeelimika na mwenye maarifa, stadi, umahiri, uwezo na mitazamo
chanya ili kuweza kuchangia katika kuleta maendeleo ya Taifa.
Dkt. Akwilapo ameongeza kuwa jumla ya
shilingi Bil. 93.8 zimetumika kuimarisha miundombinu katika shule 588 za
msingi na sekondari zikiwemo shule kongwe, ambapo serikali imeongeza mikopo ya
elimu ya juu kutoka Tzs Bil. 424.7 mwaka 2018/2019 hadi Tzs Bil. 450 mwaka 2019/2020.
Akielezea kuhusu makusanyo ya
madeni ya wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu amesema yameongezeka kutoka Tzs
Bil. 21.1 mwaka 2014/2015
hadi Tzs Bil. 183.2 mwaka 2018/2019 ambapo wizara inafanya mapitio ya sera ya
elimu ya mwaka 2014 ili kuifanyia maboresho na kuendana na wakati.
Amewaasa viongozi wa sekta ya elimu
kushirikiana na waandishi wa habari kwa uwazi ili wananchi wapate taarifa za
sekta ya elimu zenye usahihi na kwa wakati.
Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo katikati akimsikiliza Katibu Mtendaji
wa NACTE, Dr. Adolf Rutayuga wakati alipokuwa akitoa salamu zake za
ukaribisho katika taasisi hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia Bi.Sylivia Lupembe akizungumza na kumkaribisha
Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard
Akwilapo ili kuzungumza na wahariri wa vyombo vya habari.
Ignas Anthony Chonya Mratibu wa Mradi wa TESP
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia akizungumza katika kikao hicho
kilichoshirikisha wataalam na wakuu wa vitengo kutoka Wizara hiyo na Wahariri
wa vyombo vya habari.
Mhariri Mkuu wa Clouds Media na Mwenyekiti wa
Chama cha Waandishi wa habari wanawake TAMWA Bi. Joyce Shebe akitoa shukurani
zake kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt.
Leonard Akwilapo kufuatia kikao hicho.
Makuru Petro Kaimu Mkurugenzi wa Sera na
Mipango Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia akiwasilisha mada ya sera na
mipango ya wizara hiyo katika kikao hicho.
Dkt. Lyabwene Mtahabwa Kamishna wa Elimu
akiwasilisha mada kuhusu elimu ya Awali wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya wakuu wa vitengo na wahariri
wakifuatilia mjadala huo.
Picha mbalimbali zikionesha wahariri wa vyombo
vya habari mbalimbali wakiwa katika kikao hicho.
No comments:
Post a Comment