Na
Alodia Dominick, Bukoba
Halmashauri
ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa lishe
wameweka mkakati wa kuanzisha klabu za lishe katika shule za msingi na
sekondari ili kutoa elimu kwa kundi la vijana barehe kutokana na kundi hilo
kuwa na mahitaji makubwa ya ki lishe.
Hayo
yamebainshwa na Afisa lishe wa wilaya hiyo Desdery Karugaba kwa kushirikiana na
wadau mbali mbali wa masuala ya lishe katika kikao cha kamati ya lishe cha
wilaya hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/20 kilichofanyika katika ukumbi wa
Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera.
Karugaba
kwa kushirikiana na wadau wa kikao hicho ikiwemo Idara ya Elimu wamepanga
mikakati kuanzisha klabu za lishe katika shule za msingi na sekondari kwa
kushirikiana na wadau mbali mbali ili kutoa elimu hasa kwa kundi la vijana
barehe kutokana na kundi hilo kuwa na mahitaji makubwa ya ki lishe.
Ameongeza
kuwa, halmashauri hiyo imefanikiwa katika mpango wa lishe kwa makundi ya watoto
wachanga, wajawazito isipokuwa kundi ambalo limesahaulika ni vijana barehe ambalo
ni eneo muhimu kwa kizazi kijacho.
Akitaja
kundi hilo amesema Vijana barehe ni kundi lenye miaka 9 hadi 20 ni kundi ambalo
lina mahitaji makubwa ya ki lishe ambayo katika ukuaji kuna hatua mbili ambazo
binadamu anajiita.
Alisema
kundi hili ni kundi muhimu sana kwa kuwa ukuaji wake huenda kwa kasi na
kusababisha mahitaji ya ki lishe kuongezeka hivyo kundi hili lazima lipate
elimu ya kutosha ya lishe ili kujua ni vyakula gani vinahitajika.
Aliongeza
kwa kusema kuwa, katika ukuaji kuna hatua mbili ambazo binadamu anakua kwa
haraka sana ambapo kwa upande wa watoto wa kike ni kipindi ambacho mtoto
anaanza kuingi kwenye hedhi hivyo hupoteza damu na kuwa watendaji wa vijiji
wanapaswa kuweka nguvu kubwa kuhakikisha wanajadili na kufanikisha suala la
lishe katika maeneo yao kwa kuitisha mikutano ya hadhara.
Naye
Sr. Margareth Ishengoma amesema ushirikiano wa kina unatakiwa ili kuhakikisha
suala hilo linafanikiwa mara moja.
No comments:
Post a Comment