Thursday, October 10, 2019

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BARABARA TABORA- KONGA -MPANDA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wengine, akikata utepe kuashiria ufunguzi
wa Stendi Kuu ya Mabasi Mizengo Pinda nje kidogo ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Tanzania
Dkt. Alex Mubiru kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Tabora-
Koga-Mpanda 342.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami. Wengine
katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kulia Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale wa kwanza kulia,
Waziri wa Madini Doto Biteko, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey
Mwanri, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera, Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe pamoja na viongozi wengine.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea nje ya lango kuu ya Stendi hio ya mabasi kuzungumza na wananchi mara baada ya kuifungua.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kufungua stendi hio ya mabasi.
 

Sehemu ya Barabara ya Mpanda –Stalike iliyokamilika
kujengwa kwa kiwango cha lami.
PICHA NA IKULU.


No comments:

Post a Comment