Tuesday, October 29, 2019

KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA WATU 11 WALIOKUFA KWA MAJI.

 
MBUNGE wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete, (kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe.
............................................
Na shushu Joel

MBUNGE wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete, amewaongoza viongozi wa serikali na wananchi mbalimbali katika mazishi ya watu 11 katika kata ya Msata.

Watu hao wamekufa kutokana na ajali mbaya walioipata walipokuwa wakisafiri kuelekea Tanga na gari lao aina ya noah kutumbukia darajani na wote kupoteza maisha.

Alisema kuwa ajali hiyo imetokea maeneo ya mpakani mwa jimbo la chalinze na handeni ambapo gari yao ilianguka mara baada ya daraja dogo kutumbikiwa mtoni.

Aliongeza kuwa kuna familia moja ya watu sita na mtumishi mmoja wa halmashauri ya chalinze aliyefariki na familia yake ya mama na watoto 3.

Aidha alisema kuwa vifo hivi ni pigo kwa taifa na masikitiko ya hali ya juu.

"Nimesononeshwa sana na tukio hili jana tu nimezika ndùgu zangu 6 wa familia moja Leo tena nazika mtumishi wa halmashauri yangu ya chalinze ambaye alikuwa ni afisa uchaguzi , mke wake na watoto wake 3 inasikitisha sana" alisema Kikwete.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya handeni Godwin Gondwe ambaye tukio hilo limefanyika kwenye eneo lake amewataka wananchi kuendelea kuwa na imani na serikali yao kwani ipo pamoja kwa kila jambo.

Aidha amempongeza mbunge wa chalinze kwa kushiriki katika tukio hilo kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

Naye mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa pwani ambaye ni mkuu wa wilaya ya kisarawe Jokate Mwegelo amewapa pole wafiwa na kuwahakikishia serikali ipo nao kwa kila jambo.

Aliongeza kuwa ameushukuru uongozi wa wilaya ya handeni kwa ushirikiano mkubwa waliouonyesha katika kuwasaka na kuokoa miili ya wananchi wenzao.

Kwa upande wake msemaji wa familia Abdullah Semiono ameipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli kwa kusimamia na kuhudumia msiba wa ndugu zake.

Aliongeza kuwa kuna waliotangaza vibaya juu ya tukio hili kuhusu serikali naomba wabezwe kwani serikali imetusimamia na kutuhudumia kwa kila kitu kwenye msiba wetu.

"Niaze kwa kumshukuru mbunge wetu Ridhiwani Kikwete,mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gongwe na kisarawe Joketi Mwigelo kwa ushirika wa dhati katika tukio hili" Alisema
 
 MBUNGE wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete (kulia) akisalimiana na Kaimu Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, ambae ni Mkuu wa wialaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo ambaye katika mazishi hayo alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

 Majeneza yaliyobeba miili ya marehemu hao

No comments:

Post a Comment