Naibu Waziri wa Kilimo Mh.Omary Mgumba akifungua
mkutano wa kuwasilisha kwa Wabia wa Maendeleo mpango kazi wa utekelezaji wa
mkakati wa kitaifa wa kupunguza Upotevu wa Mazao kwenye mkutano uliofanyika
ukumbi wa Kizenga Makumbusho jijini Dar es salaam.
..............................
Inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2050
kutakuwa na watu bilioni tisa (9) hivyo mahitaji ya chakula yanakadiriwa kuwa
asilimia 60 zaidi ya ilivyo sasa.
Hayo yamesemwa jana septemba 30, 2019 na Naibu Waziri wa
Kilimo Mh. Omary Mgumba, katika hutuba aliyoitoa kwenye ufunguzi wa mkutano wa kuwasilisha kwa Wabia wa
Maendeleo mpango kazi wa utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa kupunguza Upotevu
wa Mazao.
Akizungumza katika ufunguzi huo,
Mh. Mgumba amesema Mahitaji ya chakula yanakadiriwa kuwa asilimia 60 zaidi ya
ilivyo sasa.
“Katika kukabiliana na changamoto
hiyo, Umoja wa mataifa umedhamiria kutokomeza baa la njaa kwa kuhakikisha kuna
usalama wa chakula na lishe, kupunguza upotevu wa mazao na kukuza kilimo
endelevu ifikapo mwaka 2030”. Alisema Mh. Mgumba.
Aidha, Mh. Mgumba alisema kuwa mkazo
umewekwa katika kuongeza uzalishaji wenye tija wa mazao ya chakula ili kufikia
malengo endelevu.
” Udhibiti wa upotevu wa mazao ya
chakula ni suala muhimu na la kipekee ambapo linapaswa kupewa kipaumbele ili
kufikia malengo hayo”. Alieleza Mh. Mgumba.
Pamoja na hayo, Mh. Mgumba alisema
kuwa Usalama wa chakula ni moja ya lengo kuu la Wizara ya Kilimo katika
kuchochea ukuaji wa Uchumi wa Viwanda ili kutekeleza agenda kuu ya serikali ya
Awamu ya Tano inayoongozwa na Mh. Dkt. John Pombe Magufuli.
Bw.
Clespin Josephat Mratibu wa Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu Tanzania (TANIPAC)
akizungumza katika mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kizenga Makubusho
jijini Dar es salaam.
Felix Bachmann Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la
HELVETAS akiwasilisha mada katiia mkutano huo.
Naibu Waziri wa Kilimo Mh.Omary Mgumba akwa
katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo uliofanyika ukumbi wa
Kizenga Makumbusho jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment