Migomba
ikionekana kuanguka baadaa ya mvua iliyoambatana na upepo kunyesha katika wilaya
ya Karagwe mkoani Kagera hapo jana Oktoba 12, 2019.
........................................
Na
Alodia Dominick, Bukoba.
Mvua
za kimbunga zilizonyesha zikiwa zimembatana na upepo mkali zimeezua nyumba sita
na mashamba ambayo idadi yake haijafahamika mara moja katika kitongoji cha
Misha kata ya Rugu wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.
Diwani
wa Kata ya Rugu Adirian Kobushoke amethibitisha kutokea kwa kimbunga hicho na
kusema kuwa kimetokea jana Oktoba 12, 2019 majira ya saa tisa alasiri
iliponyesha mvua kubwa ikiwa imeambatana na upepo mkali na kusababisha migomba
na mikahawa kuanguka chini na nyumba sita kuezuliwa na upepo.
Kobushoke
amesema, bwana shamba wa Kata ya Rugu akishirikiana na afisa mtendaji wa Kata
hiyo wanafanya tathimini ya migomba na mikahawa iliyoanguka ili kubaini thamani
halisi ya hasara iliyowakumba wananchi wa kitongoji cha Misha ni pamoja na
thamani ya nyumba zilizoezuliwa na upepo.
"Kimbunga
hicho licha ya kuangusha migomba na mikahawa pamoja na kuezua nyumba hakuna
madhara mengine yaliyotokea kwa wananchi". Alisema Kobushoke.
Mmoja
wapo ambaye nyumba yake imeezuliwa na upepo Vumilia Endrew amesema yeye ana
familia ya watu nane, yeye na mkewe naa watoto sita, baada ya nyumba yake
kubomoka jana ametoa taarifa katika uongozi wa kitongoji na kijiji pamoja na
kata na kupewa turubai ambayo imemsaidia kwa ajili ya makazi tangu jana wakati
jitihada nyingine zikiendelea kufanyika.
Baadhi ya nyumbazilizo ezuliwa mapaa yake katika kitongoji cha Misha kata ya Rugu wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.
No comments:
Post a Comment