Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi (kushoto) akimkabidhi ilani ya Uchaguzi ya CCM, Mkuu mpya wa Wilaya ya Nachingwea Hashimu Komba, mara baada ya kumuapisha.
Mkuu mpya wa Wilaya ya Nachingwea Hashimu Komba, akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
........................................................
Na Hadija Hassan, Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi Oktoba 23, 2019 amemuapicha Mkuu mpya wa
Wilaya ya Nachingwea Hashimu Komba huku akimtaka ahakikisha Mradi wa upanuzi wa
soko unakamilika ndani ya mwezi mmoja.
Tukio hilo limefanyika katika ukumbi
wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu huyo wa Mkoa wa Lindi kufuatia Mkuu wa Wilaya hiyo
uteuzi wake kutenguliwa hivi karibu na Mhe, Rais.
Zambi alisema ni lazima wafanya
biashara hao walioacha kutumia eneo hilo la Soko kwa muda mrefu waweze kurejea
katika maeneo yao ndani ya mwezi mmoja ili waweze kuendelea na Shughuli zao
kama zamani.
Hata hivyo Zambi pia alimtaka
Mkuu huyo wa Wilaya kwa kushirikiana na Ofisa mipango na Mkurugenzi mtendaji
Mpya wa Halmashauri hiyo HASSAN ABAS RUNGWA kupitia upya matumizi ya fedha
katika mradi wa ujenzi wa mabweni mawili ya Shule ya Nachingwea high school
kutokana na fedha za mradi huo kuisha kabla ya mradi kukamilika.
Pamoja na mambo mengine Zambi
akizungumzia kuhusu stand mpya amemuagiza kamanda wa polisi Mkoa wa Lindi
prudensiana protans, amuagize Mkuu wa Polisi Wa wilaya ya Nachingwea kutangaza
kuwa magari yote yaliyorudi stand ya zamani kuanzia oktoba 24 yarudi stand mpya.
"kama alivyosema mhe, Rais
kuwa hakuagiza watu warudi Stendi ya zamani bali tunatakiwa kuipangia matumizi
stendi hiyo, nikuagize RPC ili tusimpe kazi kubwa huyu Mkuu mpya wa Wilaya
muagize OCD wako wa kule awatangazie watu wa kule kwamba kuanzia Tarehe 24
Mgari yote ya abiria yarudi Stendi Mpya" alifafanua Zambi.
Akizungumza Baada ya tukio hilo
la kula kiapo Mkuu huyo Mpya wa Wilaya ya Nachingwea, Hashimu Komba alitumia
fursa hiyo kumshukuru Rais Magufuli kwa kumuamini na kumteuwa kushika nafasi
hiyo huku akiahidi kufanyia kazi maelekezo yote aliyopewa sambamba na kuomba
ushirikiano kwa viongozi na watumishi wenzake
No comments:
Post a Comment