Wahitimu wa darasa la saba 2019 katika shule ya Msingi ya Yemen DYCCC iliyopo Chang'ombe jijini Dar es Salaam wakiwa katika sherehe ya mahafali yao.
Makamu Mwenyekiti wa bodi ya DYCCC, Mohammed Abdallaah Bin Ishaaq, akizungumza
katika mahafali hayo.
..................................
Wazazi
na walezi wametakiwa kuwa karibu na watoto wao ili watoto waige tabia njema
kutoka kwao.
Wito
huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya DYCCC inayomiliki shule za Yemen
DYCCC zilizopo Chang'ombe jijini Dar es laam, Mohammed Abdallaah Bin Ishaaq,
alipokuwa akizungumza katika mahafali ya wahitimu wa darasa la saba shuleni
hapo.
Alisema
njia nzuri ya mtoto kujifunza ni kuwa karibu na mzazi ambapo ataweza kuiga
mambo kutoka kwa mzazi badala ya kuiga kutoka kwa watu wengine ambao watakuwa
na mila na desturi zao tofauti na zile za familia yako.
Aliongeza
kuwa, mzazi anapaswa kuwa karibu na mtoto huku akijenga nae urafiki ili mtoto
awe huru kuuliza maswali ya kujifunza na kuiga tabia njema.
Alisema
ikiwa mtoto utamkataza kitu fulani kuwa ni haramu au kina madhara, ni vyema
ukamtolea ufafanuzi na kuweka wazi madhara ya kitu hicho ili nae awe na elimu
juu ya madhara hayo jambo litakalomjengea hofu na kutokufanya kitendo hicho.
Aidha,
Mohammed Abdallaah ametahadharisha kuwa, mapenzi ya kuwa karibu na mtoto yasiwe
yale ya kumruhusu kufanya kila kitu na badala yake mzazi ndio anatakiwa kutoa
muongozo wa kitu gani mwanae afanye na kipi asifanye.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu wa shule za DYCCC, Hassan Akrabi, alisema
changamoto iliyopo sasa katika malezi ni kukua kwa teknolojia ya mitandao hali
inayopelekea vijana kuinia kwenye mitandao hiyo bila ya kuchagua kilicho
kizuri.
Aliongeza
kuwa, watoto hawana upambanuzi wa kujua vitu vibaya kulingana na umri wao hivyo
wazazi wana wajibu wa kuwasimamia ili kuwaongoza kwenye matumizi katika
matumizi ya mitandao ya kijamii.
Alisema
kuwa, katika matumizi ya mitandao ya kijamii kuna faida lakini pia yapo madhara
mengi ambayo tahadhari isipochukuliwa mapema na wazaz na walezi vijana wengi
wataharibika kimaadili.
Akizungumza
kwa niaba ya wazazi, Makamu Mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo, Habibu Suluo
amewataka vijana waliohitimu darasa la saba shuleni hapo kuendeleza maadili ya
dini ya kiislamu waliyopata shuleni hapo ili wapate radhi za Mwenyezimungu,
Subhaanahuwataala duniani na akhera.
Alisema
katika jamii kuna vishawishi vingi hivyo wanapaswa kutumia akili zao kwa elimu
waliyopata kukabiliana na vishawishi hivyo na kwamba wao waendelee kuwa mfano
wa kuigwa katika jamii.
jumla
ya vijana 89 wamehitimu elimu ya msingi shuleni hapo kati yao wavulana ni 43
huku wasichana wakiwa ni 46
Mwenyekiti wa Bodi ya elimu shule za DYCCC, Hassan Akrabi, akizungumza katika
mahafali hayo.
Meneja
wa shule za Yemen DYCCC zilizopo Chang'ombe jijini Dar es Salaam, Jamila Awadhi
akizungumza katika mahafali hayo.
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo, Habibu Suluo, akizungumza katika
mahafali hayo, kulia ni Mjumbe wa Bodi, Salmeen Aljabry na kushoto ni
Mwenyekiti wa Bodi ya shule za DYCCC, Hassan Akrabi.
Makamu Mwenyekiti wa bodi ya DYCCC, Mohammed Abdallaah Bin Ishaaq, (kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya shule za DYCCC, Hassan Akrabi (kulia) wakiangalia michezo iliyokuwa ikionyeshwa na vijana wahitimu wa darasa la saba 2019, shule ya msingi Yemen DYCCC.
Wahitimu wa darasa la saba 2019 katika shule ya Msingi ya Yemen DYCCC iliyopo Chang'ombe jijini Dar es Salaam, wakionyesha michezo aina mbalimbali katika sherehe za mahafali yao.
Wahitimu
wa darasa la saba 2019 katika shule ya Msingi ya Yemen DYCCC iliyopo
Chang'ombe jijini Dar es Salaam wakiwa katika sherehe ya mahafali yao.
No comments:
Post a Comment