Na
Hadija Hassan, Lindi.
Hatimae
changamoto ya ufinyu wa jengo la kuhifadhia maiti iliyokuwa ikiikabili Hospitari
ya Wilaya ya Kilwa Kinyonga, Mkoani Lindi imepatiwa ufumbuzi baada ya kampumi ya
PAN AFRICA ENERGY kufadhili ujenzi wa jengo hilo.
Ujenzi
wa chumba hicho cha kuhifadhia maiti kinaenda sambamba na ujenzi wa Duka kubwa
la dawa litakalokuwa linamilikiwa na Hospital hiyo ya Wilaya ambavyo vyote kwa
ujumla wake vitagharimu zaidi ya shilingi milioni 361 kwa makubaliano ya
kampuni hiyo ya Gesi na Halmashauri hiyo.
Akisoma
taarifa ya mradi huo katibu wa Afya wa Hospital hiyo Zabibu Uledi mbele ya
kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Mzee Mkongea Ally kwa niaba ya
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo alisema kuwa makubaliano ya jengo hilo yalikuja
baada ya Hospital hiyo kutumia chumba kidogo cha muchwari ambacho kilikuwa
hakikidhi mahitaji kutokana na ongezeko la watu wanaohitaji huduma katika
Maeneo hayo.
Akizungumza
katika ghafla hiyo ya uwekwaji wa jiwe la msingi baada ya kutembelea, kukagua
na kuridhishwa na taarifa za ujenzi huo kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa
Mzee Mkongea Ally amemtaka mkandarasi anaetekeleza mradi huo Kuhakikisha
majengo hayo yanajengwa kwa ubora na kwamba vifaa vyote vitakavyotumika katika
ujenzi huo viwe vinapitia maabara ya Serikali ili kujihakikishia ubora wake.
Kwa
upande wake Meneja uwajibikaji wa Shughuli za kijamii wa kampuni ya Pan African
Energy Andrew Kashangaki alisema kuwa kampuni yao licha ya ujenzi wanaofadhili
katika Hospital hiyo ya Wilaya lakini pia kampuni yao kwa kuthamini afya za
Wananchi wa Wilaya hiyo pia wanafadhili ujenzi wa kituo cha Afya cha somanga
katika kata ya somanga
No comments:
Post a Comment