Na
Shushu Joel
WANAFUNZI
wa shule ya sekondari ya kijereshi iliyoko katika wilaya ya Busega mkoani
Simiyu wamemuomba mjumbe wa kamati ya siasa mkoani Simiyu Simon Songe kufikisha
salamu zao za dhati kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli kwa kitendo cha kufanya watoto wa masikini kusoma.
Wakitoa
salamu hizo wanafunzi hao katika mahafali ya kidato cha nne walisema kuwa
wazazi jambo la Rais Dkt Magufuli kuwafutia ada imekuwa ni faraja kubwa kwao na
familia zao.
Akizungumza
kwa niaba ya wanafunzi wenzake Pula John alisema kuwa wanafunzi wengi ndoto zao
ni kuja kulisaidia taifa lakini wengi wao zilizima kutokana na familia nyingi
ni masikini.
"Tunakuomba
Simon Songe kufikisha salamu zetu kwa Rais kwani wewe ni kiongozi mkubwa katika
mkoa wetu wa simiyu hivyo salamu zetu zitafika"
Aliongeza
kuwa wanampongeza Songe kwa kuthamini sherehe ya wanafunzi hao ingawa majukumu
yake ni mengi lakini amefika na kutatua baadhi ya changamoto za shuleni hapo.
Aidha
katika mahafari hayo Songe ameweza kusaidia vitu mbalimbali kwa ujenzi wa
miundombinu ya shule, jezi za michezo kwa wavulana na wasichana, mipira na pesa
taslimu.
Naye
mkuu wa shule hiyo Zakaria Miyeye amempongeza Simon Songe kwa hotuba yake ya
kuwataka wanafunzi waliopo mashuleni kutumia fursa iliyotangazwa na serikali ya
awamu ya tano ya kusoma bure.
Songe
ni kijana mwenye busara na ushauri mzuri kwa vijana hivyo watu kama hawa ni
hazina ya pekee katika taifa.
Kwa
upande wake Mgeni rasmi Simon Songe amewahakikishia wanafunzi wa shule hiyo
kuwa salama hizo zitamfikia mh Rais Magufuli bila wasiwasi.
"Nadhani
mmeona jinsi wadogo zenu wa darasa la saba walivyoutangaza mkoa wa simiyu Kwa
kuwa kumi bora"Alisema.
Hivyo
amewataka wanafunzi wote wa kidato cha nne katika mkoa wa simiyu kutumia vizuri
ubunifu wa hali ya juu unaofanywa na mkuu wa mkoa Antony Mtaka kwa kuanzisha
makambi kwa wanafunzi wa madarasa ya mitihani.
No comments:
Post a Comment